Home BUSINESS Wakaazi wa pwani Wamumiminia Sifa tele Rais Wiliam Ruto

Wakaazi wa pwani Wamumiminia Sifa tele Rais Wiliam Ruto

0

AHADI nono za Rais William Ruto kwa Kaunti za Pwani zinazidi kufufua matumaini miongoni mwa wananchi wanaodai kuwa endapo zitatimizwa, basi Ukanda wa Pwani utakuwa eneo bora la kuishi.

Katika ziara yake ya Lamu hapo jana , Rais alifichua kuwa serikali yake tayari inafanya juu chini kuboresha sekta kadhaa ambazo ni uti wa mgongo kwa uchumi wa kaunti za Pwani, hasa uvuvi.

Kwa mujibu wa Rais Ruto, takriban shilingi milioni 550 zitakabidhiwa sekta ya uvuvi kwa kaunti za Pwani kwenye ziara yake ya siku tano eneo hilo kwa minajili ya kupanua sekta hiyo muhimu ambayo imeajiri wakazi wengi huko pwani.Rais Ruto alisema baadhi ya fedha hizo zitawaendea makundi ya wavuvi, hasa kwenye kaunti za Lamu, Tana River, Kilifi, Mombasa na Kwale, ambapo makundi ya kijamii ya wavuvi huko Lamu tayari yalishakabidhiwa shilingi milioni 63 za kuboresha shughuli zao.

 

Aliwasisitizia wavuvi na watumiaji wa bahari za Pwani na Kenya kwa ujumla kuwajibika katika kuona kwamba uvuvi unapanuliwa vilivyo.Hapo jana Rais Ruto aliwapokeza mabaharia wa Lamu ambao ni manahodha leseni 300 za kutekelezea shughuli zao baharini na kujipatia pato bila kusumbuliwa.Hata hivyo alielezea kuwa mpango huo utaendelezwa kwa kaunti nyingine hadi pale mabaharia wote zaidi ya 2,000 kwenye maji ya Kenya watakapopokea vyeti hivyo vya idhini ya utendakazi wao.

 

 

Rais alikigusia suala la nyumba za bei nafuu,akisema yuko imara kushirikiana na kaunti mbalimbali nchini, zikiwemo za Pwani ili kuhakikisha mpango huo unafaulishwa.Huku akidai kuwa kufikia Desemba, yeye atarudi Lamu kuzindua mpango wa nyumba za bei nafuu,na kutaja kuwa tayari ardhi ya kutekelezea mradi huo imepatikana.Rais aligusia suala la Bandari ya Lamu na kusema serikali kuu kufikia wiki ijayo itatangaza tenda ya kimataifa ili kuwezesha bandari ya Lamu kutekeleza biashara ipasavyo, sawasawa na hadhi yake ya kuwa bandari ya pili kubwa nchini.

 

 

Previous articleKenya inatarajia kupokea Wajumbe 3 Wa Mapatanisho kati ya serikali na upinzani
Next articleAUDIO | Mzee Wa Bwax – Mapenzi | download mp3