Wajinga Sisi Lyrics – Frasha
Verse One
Hello Hello
King Kaka
Ni Frasha Hapa
Manze hii fight alone
Hauwezi toboa
So nimeamua kustand na wewe
So kabla wanisummon
Wacha nitoe yangu summon
Nasikia Waiguru ameku sue
Is this true?
Funny vile Judiciary imekuwa circus
Judge na Politicians wakiwa main acts
Mshukiwa anaachiliwa kwa bondi ya millioni mbili
Na kesi yake ni ya billioni mbili
Nani atatupigania
Hatujui maguru wa NYS
Na Ruto na makesi za shamba
Scandals za mahindi
Na story za mumias na sukari
Na hata kama wewe ni pastor unang’ang’ana
How can you have such a deceitful tongue
But sunday church bado tutajazana, wajinga sisi
Story ya SGR tuliacha kuicompare na Ethiopia
Na wale pia walikuwa wanapiga kelele
Walinyamazishwa pia
Verse Two Wajinga Sisi Lyrics
Hello, unaniskia?
System ya education
Ni ya kubebesha punda mzigo
Apo ndio mwanzo wa mtego
We go to schools to become
Educated fools with no jobs
Justice ni ya wenye doo
Lawyers nao ni mabeneficiaries of a failed system
No wonder masomo inaitwagwa system
Wajinga sisi
Na hata wakitumurder
Damu ya Sharon itatu owe bado
Siogopi kufa ju kwa system niko dead
Na bado mi si sonko
Na hakutakuwa na commission of enquiry
Wazee wapate makazi na salary
No wonder vijana wako moody daily
Wakiworry hii kesho itafika lini
Ju bado si ni wazee na ni future leaders
Verse Three Wajinga Sisi Lyrics
Hello, hello unanisikia? wajinga sisi
Daily tuko kwa mitandao IG na TWITTER
Tukionesha vile tunaishi poa
Ni kama kila mtu alitoboa
Picha kwenye hoteli na meli daily
But ukweli tuko chini tunasuffer
Vitu ni hard kwenye ground
Kwenye matanga hakuna mtu ako sad
Familia ikilia wanasiasa wanajicampaignia
Nimesaidia familia na elfu mia
Kisha makofi tunawapigia
Wajinga sisi
Itaanza kutuuma lini sisi
Itaanza kutusumbua lini sisi
Future generations ni kina nani?
Na nani watawapigania
Tunashinda tukipuliza gunia
Eeeh mungu nguvu yetu
Iilete baraka kwetu
Haki iwe ngao na mlinzi
Na tukae na undugu amani na uhuru
Bado kuwa mkenya najivunia
But nimechoka kuvumilia
Time ni ya kujipigania
Tokeni mitandaoni
Kujeni tujenge Kenya
Maovu ni maovu
Haijalishi ni nani aliyatenda
Na sitasimama maovu yakitawala
Wakiuza sura badala ya kuuza sera
Ju handouts hazitawahi kujengea barabara
Handouts hazitawahi kujengea shule
Handouts ndio kabila ya umaskini
Hallo, The number you have dialled is not interested at this time
ALSO, SING TO Wajinga Nyinyi Part 2 Lyrics – Teardrops Poet