Home GENERAL Wajinga Nyinyi 4 Lyrics – Willie Oeba, Shanki & Evansquez

Wajinga Nyinyi 4 Lyrics – Willie Oeba, Shanki & Evansquez

0
Wajinga Nyinyi 4 Lyrics

Wajinga Nyinyi 4 Lyrics – Willie Oeba, Shanki & Evansquez

Verse One – Wajinga Nyinyi 4 Lyrics

The sitting president is now sleeping
Aah aah he is sipping
Na wenye tulipea kazi ya kutupa solution
Ndio wanauliza why Kenyan’s are broke
Hii swali ni offensive kama kuenda ukambani
Kuuliza when did the rain started hitting us

Tell me, what better they are doing If not playing us
Back to basics, madeejay we need to start from the scratch
Ni kama watu wazimu wanatarget school going kids
Mtoto anakuwa mzazi for no apparent reason
Na kiongozi wako anaspeak fire anataka kuona blood shed
Ni kama akona blood vision

Justice imeenda na bei ya kuongea na mwananchi ni bubu
Walipaint mabasi za shule yellow ndio waache legacy
Lakini kwa classes rooftop na exam zote zinaleak
Nani mwingine unaangalia more better leader than you
Na profile yako ya whatsapp ni more useful than the current DP
Hiyo pesa ya kisima waliiba and that is the damn truth

Sudden death is viewed kama spoiled votes that’s the sad truth
Hakuna food shelter ama ata clothing that’s the naked truth
Mayouth hawana fare ya kuenda job interview
Politician we kile inakusumbua ni mafuta ya ndege that is the plain truth
Life ain’t easy that’s the hard truth
It is not about sucking drugs ndio inacreate mawasted youths

Nchi machef hawawezi afford ile food wanacook
Doo maoptician wanalipwa huwezi ata piga look
Kill scene to see God hata utoe tithe aje ticket ya heaven hainunuliwi my mook
Walimu wanasurvive the hire purchase na kuna vitu mob hawawezi ata book
Itakuaje cries za tajiri ni intellectual na cries za maskini kwa maskio ya justice ni kelele
Itakuwaje unabelieve in me na nikicheza kimimi unashikwa na kiwewe

Itakuwaje unaninyima opportunity ya kupata kazi lakini kwa club unataka nipewe
Itakuwaje unajaribu kugeuka kifo Kuseparate mtu na mkewe
Hii effect ya nguvu ya Thao inafika mahali nduru ya mnyonge haiwezi fika
Ballot box na DSTV zinafika mahali dishi haiwezi fika
Watoto wanalala njaa ati juu ulikunywa na pesa ya kula
Na vizuri unajua pombe haiwezi lika

Wengine wanaenda kanisa ju wanaogopa wakikufa nani atawazika
Wanasiasa pia wanadanganya si movie pekee yake
Nikutricky ata manzi yako akona manzi yake uko pekee yako
Sikuhizi ukisaidia rafiki yako pesa yako unapoteza rafiki yako na pesa yako
Wonder why hukuwa heartbroken na ile hoteli unaenda ukiwa na manzi yako
Ukiwa pekee yako we huwezi jipeleka

Unatafuta mapenzi wapi na we mwenyewe umeshindwa kujipenda
Mungu saidia hawa watu hujisaidia
akuna chakula kuna watu hata waamue kuenda msalani hawawezi kujisaidia
Kosa chakula omba mabeste watakunyima wanunue waende online wakutag
Madawa na mabeste wanashindana kukudrug
KPLC wakidhani wamezima stima hapa ndani kuna wale wakona maplug

Watoto wanaomba pesa na vikombe ukipita late night wao tu ndo watakumug
Jesus alibetrayiwa na kiss we uko hapo unajichocha ju ulipewa hug
Wajinga Nyinyi

Verse Two – Wajinga Nyinyi 4 Lyrics

Sisi ni wajinga design politicians wameiba doo za gava ndio hushinda the next elections
Just imagine corruption ndio huwafanya famous
Hatukuongea vile Kenneth alinunua wheelbarrow moja ya 100k
Ona sasa yeye ndio speaker
Mko kwa laini mnachomwa na jua mkichagua politicians walishajichagua, wajinga nyinyi
Tunasahau haraka walitudanganya wataseek justice kwa victims wa dam tragedy ya solai

So sad compensation money ililand at the wrong hands
And just like robert’s second name it was still a lie
Ju tulielect watu walibeba bible wakipledge allegiance to the country
Huku hawajui ata verse ya kwanza ya wimbo wa taifa
Vitu wanatuambia ni kama jina ya pili ya Tiwa Savage
Wanaweza fanya ushikwe na kisukari vile wanagrab shamba za miwa

Natural resources hazitunzwi uchafu imejaa kwa ziwa
This is toxic na hata ka wewe si drug user itabidi umedetox na maziwa
Hawahitaji vijiko na sahani hii ni mali ya umma inaliwa
Hawa watu wanatuona mafala independent candidate anakuja kutuomba kura
Huku amevaa pati pati hii si simplicity hii ni kama mchezo wa katii na mwananchi ndio ako katikati
Wanajaribu kutupiga  from all sides niambie nani yuko taabani

Hii gava inakula mingi but inaskia uchungu ikiproduce ka mtu amekula gwava
Serikali ikona mkono mrefu ndio maana mapolisi wanatuhanda
Mashinanai barabara ni za murram na mwakilishi wao ako Nairobi anaongea kilami
Hakuna mtu wa kutuangalia na mawatchman hawalali
Wasanii wameacha kumake good music wanashindania nani mkali
Kuna huge gap kwa social status wengine wako jangwani wanakufa ju hawana maji

Wengine wako kwa club wanakufa juu wako maji
Hawa watu wanatuambia wamepea vijana kazi na vijana hawana kazi Sikuhizi wote ni wasanii
Bei ya unga hatuna industries gava haisupport wakulima wa mchele
So utaexpect aje hii economy irise
Usijiulize kwa nini nimeshika moto ni hii stori inaniwasha
Hospitalini hatuna madawa na tuko na katiba

Country unaweza amka ukiskia njaa na ulilala kifudifudi
Mwanamke unajidai uko on dat na kazi yako ni kukula fare
Hatuna role models
Mnalalamika vijana wanatumia mihadarati
Na mheshimiwa mwenyewe project zake zinadrag
Mwananchi anavaa matambara na wao wanaongeza magari ndio wabrag

Unachukia jirani yako ju mr. politician alisema
Bado hujui si sote tukona common enemy
Utacomplain aje leader wako ni corrupt
Na pia wewe alishakubribe na noti za fifty
Country imeshindwa kulipa deni ya china
Inaeka youth akona deni ya tala na mshwari CRB

So ironic mahali unatoka kiongozi mzembe ndio amesimamia CBD
Issue zinaaffect common mwananchi zikiongelewa kwa parliament
Ndio utajua kuna serikali na opposition
Lakini ikifika kwa issue ya wao kuongezwa mishahara
Wote huwa on the same side
Wajinga Nyinyi

Verse Three – Wajinga Nyinyi 4 Lyrics

Unaweza kuwa na verses tofauti but shida ni vina
Kwa hii industry kunaweza kuwa na artist wakali tofauti but shida ni jina
Si ata majimarefu huwa tofauti but shida ni kina
Election si ya mtu mmoja ni ya watu tofauti
Solidarity ndio iwepo  lazima kuwe na akina
Sawa acha niwaelezee mambo kwa kina

Kuna history heartfelt ya Robert Ouko na Tom Mboya
But there is nothing to celebrate about China and Ngoyangoya
Tumewanyamazia for long wanaona si ni maboyaboya
Huu ujumbe ni wenu this message is foyafoya
Turkana ni kama an empty closet haina nguo but ina hanger
Waliacha kuconfirm kama employed teachers wako qualified

Sikuhizi wanaconcentrate na projects za kujenga madaraja
Incase student asipoperform anaweza fanya bridging
Unajua kwa nini tunashinda kwa most terror attacks
Ni ju magaidi wakona majeshi wengi yet saliva zetu zikona amylase
Ukiuliza politician hao huiba mara ngapi watakuambia all the time
Ni kama wameambiwa wapeane feedback ya God is good

What makes the loudest noise ni an empty debe
Walirealize tukiwapigia tutanotice how foolish they are
Thats why siku za campaign wao huamua kujipigia debe
Yes job ziko nyingi but the question is where?
Hii dunia huwezi jiinua pekee yako ata basement ya pyramid ni square
Magwiji wa hesabu wanajua hii life inataka maujanja

That’s why apart from bearings na logarithms pia kuna matricks
There is no difference between us when we were young and our economy coz we were all raised
Maleaders wapo wengi na pia kupata a good one si shida
But God tupe sign kama mwisilamu mwenye anapray hard hadi kwa foid yake kuna sijida
Tumejibeba ndogo yet tuna uwezo ya kuhandle vitu heavy
Mwanasiasa anaiba billions of money anaenda chini ya maji na hatafutwi Yet kuna Kenya Navy

Wanapelekwa kotini lakini kutoa fine ndio wamengoja ju pesa anazo
Yet kuna mwananchi anauza vitu akiwa roho juu coz kanjo wanamkula mawazo
Naweza rap kuhusu Kenya Ferry niwambie vile services zao ni mbaya
Na juu nitabonga kuwahusu nichange hadi jina nijiite Ferry Wap
Huku kama hutakufa njaa utakufa na aflotoxin
Mahali natoka street children hubebwa usiku na lorry na wanaenda kutupwa forest ya baringo

It is high time watu waanze kujua difference ya courage na maringo
Na artists should stick to their lane ju wakijoin politics they become what they sing about
Ona sasa Jaguar amekaa tu starehe
Ata kama mtasema ilikuwa for publicity Akothee aligive a hand huko Turkana
So ako better of kushinda msee ulichagua
Better of kushinda hao watu hupeana bursary wakibagua

Bado ata sijaongelea kuhusu public school yenye ilicollapse nikihope
Wataacha kuwa ignorant Na wataishughulikia perhaps
Bado wanatushauri tuvote na visanga vyote tumejionea dhahiri
Siku yenye mr. president atainua maisha ya hata poet mmoja
Ndio nitaamini kuna Uhuru wa mshahiri
Wajinga Nyinyi

ALSO, SING TO Kenya National Anthem Lyrics – Both Kiswahili and English

Previous articleKenya Army Ranks and Salaries, Bonuses and Priviledges
Next articleKanua Njohi Ini Lyrics – Samidoh – December 2019