Home NEWS WAGENI LYRICS – PAUL CLEMENT

WAGENI LYRICS – PAUL CLEMENT

0
WAGENI LYRICS

WAGENI LYRICS BY PAUL CLEMENT

Katika maisha yangu
Nilipokea wageni
Nikawakaribisha kwangu
Wakafanya vitu vingi

Hawakuwa wa kudumu
Walikuwa wapitaji
Ila moyo wa ukarimu
Ukanisababishia machozi

Mgeni wa kwanza
Alikuwa ni UCHUNGU
Akaniumiza akanipa maumivu
Alipomalizaa, akaenda zake

Mgeni wa pili
Alikuwa ni HUZUNI
Huyu nae
Akanikosesha furaha

Mgeni wa tatu
Alikuwa ni MAGONJWA
Akanidhoofisha, akataka kuniua
Hakufanikiwa, akaenda zake

Aliyefuata
Alininyima watoto
Jina lake TASA
Naye alipita

Mgeni mmoja
Jina lake ni MAUTI
Akamchukuwa Mtimi
Akaniachia jeraha

Mgeni mwingine
Jina lake HOFU
Hakutaka nifanikiwe
Akanipa fikra potovu

Nikajiona siwezi
Tena nitafeli
Huyo naye alipita

Hawa ni wageni
Tena wapitaji
Hawatadumuu
Watapitaa

Hawa ni wageni
Tena wapitaji
Hawatadumuu
Watapitaa

Hakuna jambo
Lolote ngumu
Litakalo dumu
Kwenye maisha yako

Ila yote yatapita
Na yakishapita
Hayatarudi tena

Tough times never last
But tough people do

Mapito sio mambo magumu
Unayopitia kwenye maisha yako
Ila mapito ni mambo magumu
Yanayopita kwenye maisha yako

Ndio maana tuyaita mapito
Kwa kuwa yanapita tu
Na yanapita kwenye maisha yako
Na yakishapita hayawezi kurudi tena

Magonjwa
Hawa ni wageni
Tena wapitaji
Hawatadumu, watapita

Uchungu
Hawa ni wageni
Tena wapitaji
Hawatadumu, watapita

Mateso
Hawa ni wageni
Tena wapitaji
Hawatadumu, watapita

Hawa ni wageni
Tena wapitaji
Hawatadumu, watapita

WAGENI LYRICS BY PAUL CLEMENT

ALSO, SING TO – Nampenda Lyrics – B2K