Home NEWS Uwanja Wa Shule Ya Gatina Kukarabatiwa Kwa Sh23 Milioni

Uwanja Wa Shule Ya Gatina Kukarabatiwa Kwa Sh23 Milioni

0

Uwanja wa shule ya Gatina kukarabatiwa kwa Sh23 milioni – Taifa Leo

UWANJA wa michezo wa Shule ya Msingi ya Gatina katika eneobunge la Dagoretti Kaskazini utafanyiwa ukarabati utakaogharimu Shilingi milioni 23.Akitangaza habari hizo Jumapili baada ya kumalizika kwa Mama Dago Super Cup, Mbunge wa eneo hilo, Beatrice Elachi alisema vipaji vingi vimezimwa na ukosefu wa viwanja vya kutosha.

Mwanasiasa huyo aliahidi kushirikiana na Serikali ya Kunti ya Nairobi kuhakikisha ardhi ya umma iliyonyakuliwa katika sehemu hiyo imerejeshwa mara moja.Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi aliyekuwa mgeni wa heshima wakati wa fainali hizo, alisema soka ndio mchezo unaopendwa zaidi kote duniani, na unapaswa kuheshimiwa.Timu 32 za wanaume zilishiriki katika mashindano hayo, pamoja na nyingine sita za wanawake, ambapo timu ya FIFA Best ikiongozwa na aliyekuwa beki wa kimataifa Wesley Onguso ilitwaa ubingwa wa taji la wanaume baada ya kuchapa Kabiro Youth 3 kwa 1.

Uwanja wa shule ya Gatina kukarabatiwa kwa Sh23 milioni – Taifa Leo

Diwani wa Gatina Ken Swaka, Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi, na Mbunge wa Dagoretti Kaskazini Beatrice Elachi wakati wa kupeana tuzo kwa washindi wa fainali za Mama Dago Super Cup katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Gatina mnamo tarehe 23 mwezi huu.Kikosi hicho kilichojumuisha mastaa kadhaa walioichezea klabu kubwa nchini kilipata Shilingi laki moja[100,000] kutoka kwa mdhamini wa mashindano hayo, Elachi, mbali na zawadi nyingi za pesa kutoka kwa viongozi wengine akiwemo Wanyonyi na Gavana wa Nairobi Johnston Sakaja aliyetuma zawadi yake kupitia kwa msimamizi wa Bodi ya Kutoa Leseni ya Pombe eneo hilo, Francis Onyango.

Kabiro walipokea Shilingi 50,000 kwa kumaliza katika nafasi ya pili, wakati Pirates FC na Dago Mixed zikipata Shilingi30,000 na Sh20,000 kwa kumaliza katika nafasi ya tatu na nne mtawalia.Hafla ya kuwatuza washindi mbalimbali kwenye fainali ya Mama Dago Super Cup katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Gatina mnamo jumapili wiki iliyopita. FIFA Best waliwatandika Kabiro Youth 3-1 kwenye mechi ya fainali.

Previous articleMabunge Ya Kenya Na Australia Kushirikiana Kiutendakazi pamoja
Next articleBREAKING: ONGOING COUP IN NIGER AS PRESIDENT MOHAMED BAZOUM IS DETAINED BY HIS OWN GUARDS.