Ujitume Lyrics – Ally Mahaba Ft Akeelah – Download Mp3 Audio
Verse One
Mume wangu
Kama leo huendi kibaruani tuonge
Mi na wewe tuyaweke sawa
Mambo yetu yaende
Unasemaje baby, Umenisikia
Kwanza kaniletee begi, za wapi tena
Nataka niwahi kule
Usije kanichelewesha bure bure
Kutoka kwa ni alfajiri, umelewa
Kurudi usiku siri siri, umechelewa
Humu tunaishi wawili
Ama unaishi pekee yako
Haiya nakaa chini
Unachomaanisha ndio nataka, nielewe
Mi najuwa unataka tugombane umenichoka
Yaani wewe
Huko ulipo wewe mimi sipo tumeelewana
Kutwa madeni na huishi mikopo
Mwanamume
Chorus
Inachosha, inachosha inachosha
Usiseme hivyo
Inachosha, inachosha inachosha
Usinifanye hivyo
Nataka ujitume, nitajituma
Wewe ndo mume, sawa mama
Maisha yasigume gume
Ndio nitakuelewa
Verse Two
Kuipata kazi sio rahisi mke wangu
Maisha yapo kama ngazi
Kuipanda mpaka atake Mungu
Naelewa
Kweli huwezi kupata chochote
Mpaka akupatie mungu
Bila juhudi zako je we
Utalipataje fungu
Unaniona mi kuwa sipendi kazi, sio kweli
Mimi ndio kichwa cha familia
Kuhangaika popote mi niko radhi, nisifeli
Baby nitapata vumilia
Si uende Uarabuni ukajaribu bahati yako mwenzangu
Mazonge ya viziuzi ubishi wako waovunja moyo wangu
Huko hakuna lolote pamoja na mihangaiko yao yote, ndio maana
Na ujanja wao wote pesa wanazimaliza madem zote, hapana
Basi kaa wewe nyumbani nami nitoke nikahangaike
Mwanamume unapenda ushindani
Nami nifanyeje mtoto wa kike
Chorus
Inachosha, inachosha inachosha
Usiseme hivyo
Inachosha, inachosha inachosha
Usinifanye hivyo
Nataka ujitume, nitajituma
Wewe ndo mume, sawa mama
Maisha yasigume gume
Ndio nitakuelewa
Inachosha, inachosha inachosha
Inachosha, inachosha inachosha
Nataka ujitume, nitajituma
Wewe ndo mume, sawa mama
Maisha yasigume gume
Ndio nitakuelewa
Ujitume Lyrics Credit – Ally Mahaba and Akeelah
ALSO, SING TO – Chukua Lyrics – The Mafik Ft Natacha – New Song 2020