Sonona Lyrics – Susumila Ft Mbosso
Sonona Lyrics Verse One
Siku moja moja
Ukipata nafasi tukumbukane
Nitalipa bodaboda
Acha na mwendo kasi usijibanebane
Aha, ewe binti maringo
Sijui wanisikia
Pendo lako nicheze bingo
Huenda nikajishindia
Mwenzako bado niko single
Pendo limenichachia, Aaah
Uwe suka niwe tingo
Niyoyoe abiria
Nafsi unainyong’onyeza, Aaah
Nahisi la moyo shambulio, Aaah
Nifanye chipsi chombeza, Aaah
Japo unionje onje mwenzio, Aaah
Chorus
Penzi linanilegeza
Sonona, sonona
Eti lini utapata nafasi?
Sonona, sonona
Oooh beiby yoyo, nambie basi Sonona, sonona
Nafsi nyonge, naishi kwa wasi wasi Sonona, sonona
Beba wangu moyo, mwepesi ka karatasi Sonona, sonona
Sonona Lyrics Verse Two
Mwaga wino
Wa kalamu ya penzi langu
Chimba shimo
Unizike kabla ya siku yangu
Hakuna asiyejua
Matatizo ya moyo ukipenda
Unanifanya mwanasesere
Kunichezesha
Mi muoga macho usoni
Nisijeshikwa na kwikwi kimasihara
Sema niandae vipopconi
Unyonye na vipipi vya duara
Nafsi unainyong’onyeza, Aaah
Nahisi la moyo shambulio, Aaah
Nifanye chipsi chombeza, Aaah
Japo unionje onje mwenzio, Aaah
Chorus
Penzi linanilegeza
Sonona, sonona
Eti lini utapata nafasi?
Sonona, sonona
Oooh beiby yoyo, nambie basi Sonona, sonona
Nafsi nyonge, naishi kwa wasi wasi Sonona, sonona
Beba wangu moyo, mwepesi ka karatasi Sonona, sonona
Verse Three
Uje, Uje Uje beiby, Uje Uje Mombasa wakuone
UjeUje Uje darling, Uje Uje Nairobi wakuone
Uje, Uje Uje beiby, Uje Uje Dar es Salaam wakuone
Uje, uje beiby 001 akuone
Credit: Susumila Ft Mbosso
SING TO: Kesi Lyrics – King Kaka Ft Kelechi Africana – New Song 2020