Home NEWS Soccer Assassins Wawanyoa Solasa Queens Bila Maji

Soccer Assassins Wawanyoa Solasa Queens Bila Maji

0

Soccer Assassins waliwanyorosha Solasa Queens bila huruma, kwa kuwapiga mabao matano kwa moja kati ya mechi ya Zoni B ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Divisheni ya Kwanza mnamo Jumatano.Mechi hiyo ya raundi ya 21, ilisakatwa katika uwanja wa Chambiti Primary mjini Luanda, Kaunti ya Vihiga.

Mshambulizi wa Assasins Charity Midewa alicheka na wavu mapema kipindi cha kwanza,  kabla ya Valarie Nekesa  kufunga mabao manne dakika ya 43’, 55’, 76’na 86.Nekesa ndiye mfungaji bora Zoni B akiwa na mabao 25.Bao la pekee la Solasa lilipachikwa wavuni na Joan Onyuna kunako dakika ya 17.Assassins wamesalia na nafasi ya nne na alama 45 sawia na Kisped Queens lakini wanatofautiana kwa idadi ya mabao.

Hata hivyo assassins wako na alama tatu nyuma ya vinara wa ligi Bungoma Queens.Kocha wa timu ya Soccer Assassins Nickson Muleri hakuficha furaha yake baada ya ushindi huo.Ushindi huo, umefufua matumaini yao ya kujiunga na Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) msimu ujao.

Solasa nao wako kwenye hatari ya kushuka daraja katika nafasi ya tisa na alama 18. Wamecheza mechi 21, wakapata ushindi mara sita, sare tatu na  kupoteza mechi 12.Raundi ya mwisho ya mechi za msimu wa mwaka wa 2022/23 itachezwa wikendi hii.Ambapo Kibera Soccer Women ya Zoni B ndio timu ya pekee ambayo imejiunga na KWPL.

 

Leave a Reply