Home NEWS Sinaga Swagger 4 Lyrics – Young Killer Msodoki – New Song

Sinaga Swagger 4 Lyrics – Young Killer Msodoki – New Song

0
Sinaga Swagger 4 Lyrics

Sinaga Swagger 4 Lyrics

Introduction

Ni kijana aliyepitia makubwa
Kwenye safari yake ya mafanikio
Ukizungumzia kukesha usiku
Kutafuta nafasi za  kuperform
Bro naomba nichane

Kukataliwa kwenye jamii
Na watu kumwaminisha kuwa hawezi
Na mbaya zaidi hata familia yake
Walikosa imani juu ya kipaji chake

Na kumuusia asome sababu muda mwingi
Alikuwa akionekana akideal na muzuki
Lakini, siku zote Mungu huwa
Hamtupi mja wake

Baada tu ya kupata nafasi
Aliitumia ipasavyo
And now  it’s proof to the world
The real meaning of a Young KILLER

Verse

Zinazofanya tugombane ni doh
Mpaka tunachukiana na mwisho tutoane roho
Kujifanya magangster kumbe ndani bishoo
Kupandishana mapresha kuua shingo na roho

Nilifika mchanaji mmoja matata
Hapo through-back ya Tabata
Pindi ya mambo ya Basata
Nilijua mlipata hii mkasema(Aaah sema weee)
Kwenye frame ni mdogo wasitune paja
Wambie madogo waache nyodo
Bro wao wasipompenda kaja

Haina haja kuleta jam jam zama hizi
Kumwambia nyani asali ni tamu kuliko ndizi
Kumgombanisha mvivu na usingizi
Yaani kucheka kwa furaha
Na mhalifu wako wakati wa fumanizi
That’s easy brother mambo ya trending
Sorry for long time now nothing change

Leo shetani kachelewa kuamka
Kwa hiyo mapema yale mambo makuu mawili
Na mkuu ndio kasema
Sio kesi kurefresh na kuinvest
Inadepend na pocket yako
Ila hatukopeshi na hatukeshi
Kuna muda wa mapenzi na business
Na ucheshi na kudance na mabeste na mafifa
Na mepesi eyoo majani yaani

Niwe majani mpande mawe
Niache mali shambani
Nikatafute kwenye changalawe
Kazeni kumtoa Messi LaLiga
Aje kucheza aje kucheza kikapu

Tuweni sharp rasta supu inanywewa ikiwa moto
Mimi ni kikipaka hapa hata ukikaa ufukweni joto
Nilikuwa msoto mwanzo nakumbuka mama alilia sana
Akanambia vumilia chana

Elimu dunia sio elimu ya kupuuza
Sio kila baya baya mengine mabaya yanafunza
Mwanafunzi ukifanya kitu ambacho
Hakija nifurahisha kwenye macho
Nakupiga hata Kawa mwalimu mkuu mama ako

Sikosi kugusa legeza chujio chicha zipite
Alafu nipe heshima sio mpaka nife mnizike
Na mliziba matundu yote nisipite
Msijali nitaombea Mungu hiyo dhambi asiandike

Wengi wanafurahi ninapo anguka
Hawapendi nikamate line
Acheni wanikazie ili… wengine washine
Ila mnanicompare mi na watoto wa kuja

Ni kutoa ndogo wakati una bata ni likubwa
Yaani ishindane na muda hata uwe nunda hushindi
Utavuga tu kwa wahuni alafu kwa mchumba haudindi
Na siku ntayo shindwa na mapimbi

Haki natembea nakunya toka
Mwanza kuja Dar mpaka Lindi
Nasishindwi kubeba jamii kujiamini
Napita zzzz zaidi ya dawa ya ukimwi

Mimi mtu mpole wewe aka mshamba kabambe
So ukijifunika blanketi alafu ukajamba jipambe
Eti ujimiz na watoto wa fisi alafu upitwe na ibilisi
Yaani uende urudi unamtaka Shishi
Ivi unahisi kirahisi uchebe utakuchekea
Si sawa ung’oe jino alafu utembee unachechemea

You will cry when am dying nimjue friend
Kama kusubui hakupendi, all eyes on me
If you love me, love me and show me
Life is a lesson na sina test for me

Kama hamjui mnapokwenda kwa hiyo
Sehemu mliokuepo mtahisi mmefika
Ni funzo hii sauti inaposikika
Japo inaua na kuzika
Tafuteni mikwanja mtadhalilika
Asanteni na poleni kwa pilika, Hiii hahahahha

Right now you already know who I am
Big shout out to all haters and money makers
Lengo letu si kuishi milele
Ni kufanya vitu vitavyoishi milele
Mambo mazuri yako mbele kwa mbele
Usikate tamaa msela ongeza misele

I told you, not funny
Hey leaders this time to wake up
Cause Young Killer Msodoki hahahaha
Ujue mimi sinaga swagga kabisa yaani
Eeh natoka Mwanza, Mwanza eeh Mwanza
Kwani vipi?

Sinaga Swagger 4 Lyrics Credit – Young Killer Msodoki

ALSO, SING TO – Bachela Lyrics – Queen Darleen Ft Lava Lava – New Song 2020

Leave a Reply