Home GENERAL Simu Lyrics – Goodluck Gozbert

Simu Lyrics – Goodluck Gozbert

0
Simu Lyrics

Simu Lyrics by Goodluck Gozbert. Download Audio

Verse One

Hello Baba ni mimi mwanao
Hii namba nimechukua Jeremiah hapa
Inasema niite nitakuitikia
Nitakuonyeshe magumu usiyo yajua mwanangu

Ya leo simu yangu hii
Napiga kwa imani tu
Nakuomba sikiliza Daddy
Naumia moyoni

Unaweza tunusuru na hili na hili
Manabii wale Baba ungewaambia kuna Corona
Au tunadanganywa ni bandia wanaonaga
Je umekaa kimya ukitazama wanayofanya

Mbona mwaka jana walituambia
Huu ni mwaka wa Bwana
Tumekaa mwaka ulianza shwari
Sasa hivi hatuelewi

Kila saa alama ya hatari
Ni mbaya habari
Wamekufa saba, walikufa sita
Mara ooh mnadanganywa wamefika kumi

Chorus

Mmmh acha ni sanitize
Ooh barakoa kidogo, nisishike pua
Mmmh acha ni sanitize
Ooh barakoa kidogo, nisishike macho…

Wakati nasubiri iii…

Verse Two

Heri matajiri tajiri
Wanaweza kununua mask
Wengine hizo pesa
Ndo tunategemea tule

Mama mama, ah muda wote ni presha
Maana watoto wake maisha ndo wanatafuta
Kwa siku kupata kwa siku tumezoea
Hatuna maisha kabisa ya akiba

Usipotuhurumia wewe ndo tumekwisha
Usipotuhurumia wewe ndo tumekwisha

Niliongea na waombaji
Nikawaambia tusiache kuongea
Maana adui ametumia mabaya mmh
Mi nakuamimi kuamini Baba
Mi nakuamimi mi kuamini

Chorus

Mmmh acha ni sanitize
Ooh barakoa kidogo, nisishike pua
Mmmh acha ni sanitize
Mmmh barakoa kidogo, nisishike macho…

Wakati nasubiri iii…
Wacha ni sanitize
(Asante)

Simu Lyrics by Goodluck Gozbert

ALSO, SING TO – Najiuliza Lyrics – MATTAN

Previous articleNajiuliza Lyrics – MATTAN
Next articleKilangakomo Lyrics – ASLAY