Safina Lyrics – Stamina Ft Barnaba
Safina Lyrics Verse One
Halleluyah, Halleluyah Halleluyah, Halleluyah
Halleluyah, Halleluyah Halleluyah, Halleluyah
Baba kabla haujashusha gharika kwa nchi nzima
Umenituma dumu mwanao nije nijenge safina
Napo sema Mungu ni mkubwa, ni ukweli sio poyoyo
Umemfanya hadi kiziwi anaskia mapigo ya moyo
Dini sku hizi zinavuma kwa upepo wa kisulisuli
Sioni ibada wanashindana kuvaa vizuri
Safina haina nafasi kwa watumishi mabishoni
Ndio maana siingizi wachungaji maana watakula kondoo
Umenipa madada mnnajishoot uchi sio poa
Umenipa makaka ambao wengine makaka poa
Mwanamke kuwa mwanaume wa mwanamke asiye na mume
Ni mwanaume tena wa kiume kuwa mwanamke wa mwanaume
Shuleni hawafundishwi somo linaloitwa utajiri
Bali dhamani ya x ambayo mtaani haiwapi dili
Wacha watoto waje kwako ila kwa mwendo wa polepole
Wakumbuke tu, mkono wa sweta haunaga vidole
Chorus
Lalala.. Kikubwa naomba Mungu
Aninusuru na maisha yamezidi kunichanganya
Naitazama dunia
Wanakondoo na waumini kwenye safina ndo wanazama
Oooh Jah Jah bless
Jah Jah bless , uuu yeah yeah yeah yeah yeah
Oooh Jah Jah bless
Yes sir!
Safina Lyrics Verse Two
Kwenye mapenzi washenzi wanaenzi ilimradi
Ukiitwa mpenzi bila pesa we ni mpenzi mtazamaji
Unaeza ukafa leo, wanawe wakalia usiku na mchana
Ila cha ajabu mkeo, siku ya matanga kapata bwana
Ila Baba, samahani naomba nikuulize
Najua una mambo mengi na kimtindo uko bize
Ulisema tuzaliane ili tujaze dunia
Sasa ugumba na utasa uliweka wa nini? Nafikiria
Anakamata bodaboda hajavaa helmet why?
Wakati kwa michepuko havai kinga anapiga dry
Pesa sio sabuni ya roho ni sabuni ya uchafu
Ingekuwa sabuni ya roho ingetakatisha mpaka wafu
Halafu Baba maisha ni mazoezi nguosha
Ukiona watu wanakonda ujue pesa ndo gym tosha
Malipo ni hapa hapa duniani huko mbinguni hakuna change
Usihofu safina ikijaa wengine nitawalaza kweny tenki
Chorus
Lalala.. Kikubwa naomba Mungu
Aninusuru na maisha yamezidi kunichanganya
Naitazama dunia
Wanakondoo na waumini kwenye safina ndo wanazama
Oooh Jah Jah bless
Jah Jah bless , uuu yeah yeah yeah yeah yeah
Oooh Jah Jah bless
Yes sir!
Safina Lyrics Verse Three
Ndoto zilikuwa pilot, piloti
(Dreams come true, dreams come true, dreams come true)
Zilifeli baada ya kulost
(Dreams come true, dreams come true, dreams come true)
Ushabebeshwa mikoba ya kiganga
Ushavunja nazi njia panda
Ushale mgongoni wakakuchanja
Lakini bado hauna doh, hauna doh doh doh…
Lakini bado hauna doh
Kikubwa naomba Mungu
Aninusuru na maisha yamezidi kunichanganya
Naitazama dunia
Wanakondoo na waumini kwenye safina ndo wanazama
Oooh Jah Jah bless
Jah Jah bless , uuu yeah yeah yeah yeah yeah
Oooh Jah Jah bless
Yes sir!
Oooh Jah Jah bless
Halleluyah, Halleluyah Halleluyah, Halleluyah
Halleluyah, Halleluyah Halleluyah, Halleluyah
ALSO, SING TO Mawe Lyrics – Nyandu Tozzy Ft Rayvanny & Mr Blue