Home GENERAL Sabuni ya Roho Lyrics – Best Naso – New Song

Sabuni ya Roho Lyrics – Best Naso – New Song

0
Sabuni ya Roho Lyrics

Sabuni ya Roho Lyrics – Best Naso

Verse One

Wanasema kwenye dunia
Ukiwa na pesa shidaa
Wanasema kwenye dunia
Ukiwa na pesa utanyoa
Unaweza fanya lolote
Ukatukana yoyote
Na watu wakasema sawa

Unaweza fanya chochote
Na ukampiga yoyote
Na bado akasema sawa
Yarabi tustahili
Wake za watu wanasaliti
Ndoa kwa sababu ya pesa
Yarabi tustahili
Ona maskini wanakosa haki
Kwa sababu ya pesa

Misikitini kanisani wanaiuza dini
Kwa sababu yake pesa
Ya zaidi ata niliyependana naye amenisaliti
Amesema kachoshwa na shida
Na hivi karibuni anaolewa
Ooh mpenzi ndoa
Oooooo sina changu naumia

Chorus

Ooooo Pesa
Pesa sabuni ya roho
Pesa, pesa sabuni ya roho
Ooooo Pesa
Pesa sabuni ya roho
Pesa, pesa sabuni ya roho
ooooo pesa
Pesa sabuni ya roho

Verse Two

Namwona babu mzee
Anatumikishwa kazi
Na kijana mdogo
Namwona bibi mzee
Anabebeshwa mzigo
Na vijana wadogo

Naziona nchi zinapigana
Watu wanarogana
Kwa sababu ya pesa
Namwona mama anatukanwa
Tena na katoto kadogo
Kwa sababu ya pesa

Mtaani kwetu kuna wazee
Wameoa vibinti vidogo
Kwa sababu ya pesa
Ehe eti wadogo wanazaa
Hakuna anayekataa
Kila kona za mitaaa
Machokora wamezagaa

Ona wanaishi vizuri
Wale wenye pesa zao
Tena wanakula vizuri
Wale wenye pesa zao
Magari yao mazuri
Wale wenye pesa zao
Tena wanavaa vizuri
Wale wenye pesa zao

Eeeh pesa kiboko ya njaa

Chorus

Ooooo Pesa
Pesa sabuni ya roho
Pesa, pesa sabuni ya roho
Ooooo Pesa
Pesa sabuni ya roho
Pesa, pesa sabuni ya roho
ooooo pesa
Pesa sabuni ya roho

Sabuni ya Roho Lyrics Verse Three

Kama pesa isingekuwepo
Unadhani yangekuwepo
Au isingekuwepo pesa
Haya yote yangekuwepo
Hili swali jibu swali
Usiniulize maswali
Kichwa changu kinauma
Nabaki natafakari

Kama pesa isingekuwepo
Unadhani yangekuwepo
Au isingekuwepo pesa
Haya yote yangekuwepo
Hili swali jibu swali
Usiniulize maswali
Kichwa changu kinauma
Nabaki natafakari

Swali

 

ALSO, SING TO Nipende Lyrics – Rj The Dj Ft Feza Kessy – New Song 209

 

 

 

Previous articleNipende Lyrics – Rj The Dj Ft Feza Kessy – New Song
Next articleAnajishaua Lyrics – DanZak – New Hit Song