Home NEWS Nyakati Lyrics – Goodluck Gozbert – New Song Jan 2020

Nyakati Lyrics – Goodluck Gozbert – New Song Jan 2020

0
Nyakati Lyrics
nyakati goodluck gozbert

Nyakati Lyrics – Goodluck Gozbert

Nyakati Lyrics Verse One

Unaona kama kila unachoguza kimeharibika
Ujasiri wa kusema tena umetoweka
Maana kila unachosema wewe kama unakosea
Umechanganyikiwa ni mungu ajua unayopitia

Na ukisema uelezee wengi kwao ni furaha
Wewe muombe mungu ubaki kimya
Na mengi umevumilia moyo umenyong’onyea
Hapo ulipo sasa ng’ang’ania tena

Na mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako
Imani nusu ongeza utashinda
Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako
Imani nusu ongeza utashinda

Chorus

Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali mungu yuko nawe
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali mungu yuko nawe

Nyakati Lyrics Verse Two

Moyo wako una majeraha hufai
Tena unasubiri kauli ya mwisho ya mungu
Wapo wanaojua we una mtoto
Kwa kejeli wanaulizaga ana umri gani

Tena wanaojua umefukuzwa kazi
Kwa kejeli wanaulizaga bosi wako yupo
Ila nakuambia hayatodumu ni nyakati tu
Hautobaki hapo haya ni mapito

Jipe moyo tazama juu Muombe mungu ujasiri
Ni mapito tu jipe moyo mkuu
Japo huna nguvu ya kumuomba mwishie mungu
Ni mapito tu jipe moyo mkuu

Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako
Imani nusu ongeza utashinda
Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako
Imani nusu ongeza utashinda

Chorus

Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali mungu yuko nawe
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali mungu yuko nawe

Nyakati Lyrics Verse Three

Hata wakizusha maneno ya uongo Wakakuambia umemuasi mungu
Ni sawa hawajui unakopita
Wakaja na unabii wakasema umefika mwisho wako wewe
Ni sawa hawajui unakopita

Ooh wakainuka ndugu wa karibu wakakusema ovyo ovyo
Ni sawa hawajui unakopita
Ikawa kila kitu ni kimya marafiki ni kimya
Ni sawa hawajui unakopita

Kama ndoa ni yako lakini ndani ni uadui
Ni sawa hawajui unakopita
Iiii hiiii aaa

Chorus

Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali mungu yuko nawe
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali mungu yuko nawe

Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali mungu yuko nawe
Zipo nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali mungu yuko nawe

Credit: Goodluck Gozbert

ALSO, SING TO: Asiwaze Lyrics – Stamina Ft Atan – New Song January 2020