Home NEWS Nikuache Lyrics – Akeelah

Nikuache Lyrics – Akeelah

0
Nikuache Lyrics by Akeelah

Nikuache Lyrics by Akeelah – Download Mp3 Audio

Verse One

Najiona najiuliza
Kwa nini macho yangu mekundu
Kwa taarifa yako nimetoka kulia

Hivi utaniumiza hadi lini
Hili tundu la moyo wangu
Mie mwenzako nipate tulia

Japo moyoni, moyoni
Nimejawa na subira, subira
Kuishi na wewe imekuwa kazi
Naona kama inashindikana kweli

Kama siyaoni vile
Inanitia hasira
Madhila wanifanyia wazi
Kuishi nawe mi naona nishafeli

Nichambane na madem wako
Japo mi huwaga sishiki simu yako
Hivi kwa nini hawatosheki kwako
Waniandame mie

Kunigombeza we ndio zako
Kisa tu naishi kwako
Ushashukisha thamani yako
Kwangu mie

Chorus

Dawa dawa yako nikuache
Nijiweke mbali nawe
Sawa sawa yako nikuache
Kama mawingu na mawe

Dawa dawa yako nikuache
Penzi lako kaligawe
Sawa sawa yako nikuache
Mi utaniumizaa

Verse Two

Kama kufumania nimekufumania
Sana na Tiffa nikakusamehe, haijatosha
Kusudi unarudia tena kwa kutia nia
Naona sifa mwanamume, umenichosha

Sina jeuri ya kujibu mi najiliza
Mapungufu yangu bubu nakusikiza
Hunaga cha taratibu wakandamiza
Mwanamume una gubu kupitiliza

Nichambane na madem wako
Japo mi huwaga sishiki simu yako
Hivi kwa nini hawatosheki kwako
Waniandame mie

Kunigombeza we ndio zako
Kisa tu naishi kwako
Ushashukisha thamani yako
Kwangu mie

Chorus

Dawa dawa yako nikuache
Nijiweke mbali nawe
Sawa sawa yako nikuache
Kama mawingu na mawe

Dawa dawa yako nikuache
Penzi lako kaligawe
Sawa sawa yako nikuache
Mi utaniumizaa

Dawa dawa yako nikuache
Nijiweke mbali nawe
Sawa sawa yako nikuache
Kama mawingu na mawe

Dawa dawa yako nikuache
Penzi lako kaligawe
Sawa sawa yako nikuache
Mi utaniumizaa

Nikuache Lyrics by Akeelah

ALSO, SING TO – Bwana wa Mabwana Lyrics – Zzero Sufuri