Ni wakati wa kupumua kwa mama mzazi na taasisi ya matibabu baada ya mtoto aliyeripotiwa kupotea kupatikana. Maafisa wa polisi huko Voi wamemkamata Christine Kisochi, ambaye anashukiwa kuiba mtoto wa kiume aliyeripotiwa kupotea kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Moi
Kulingana na Daktari Bingwa wa moi rufaral hospital huko voi, Jeremiah Shem, mshukiwa, ambaye alijifanya kuwa mjamzito ana aliyetarajiwa kujifungua, aliingia katika wodi moja ya uzazi ya hospitali hiyo akiwa na uchungu wa uongo.Mshukiwa hiyo alidai mtoto ni wake na alijifungua Jumatatu, tarehe 10, katika Hospitali ya Jordan ya Binafsi, lakini hakuweza kutoa nyaraka, akisema kuwa zilikuwa zimepotea.
Ambrose Maundu Gerald ambaye ni baba wa mtoto huyo, alipata afueni baada ya mtoto wake kupatikana, akishukuru hospitali na polisi kwa uchunguzi na msaada wao wa kina huku mshikiwa kiwa huyo akizuiliwa katika kituo cha polisi cha Voi kwa uchunguzi zaidi.