Home NEWS Ndoa Lyrics – Bright Ft Khadija Kopa, Juma Kakere, Karen

Ndoa Lyrics – Bright Ft Khadija Kopa, Juma Kakere, Karen

0
Ndoa Lyrics

Ndoa Lyrics – Bright Ft Khadija Kopa, Juma Kakere, Karen. DOWNLOAD MP3 AUDIO

Verse One

Mwanangu vipi baba mbona kimya baba
Uliahidi jambo mbona kimya baba
Mambo ya ndoa umefikia wapi baba
Mambo yako ya ndoa umekwama wapi niambie

Nimezunguka dunia mzima
Dunia kiganja baba, nimeyaona mengi
Ya walimwengu wanasema
Bora uchague mpenzi, tofauti na enzi

Wanafanana kwa sura matendo baba nko hoi eeh
Unayempenda na kumwaza anamwaza meingine
Bila pesa umaarufu mwonekano baba we hung’oi eeh
Na kwa dunia ya sasa, nioe wapi pengine

Dunia hadaa hilo baba utambue
Muda unaenda hilo uzingatie
Mweke Maulana mbele mambo yatimie
Dhamira yako ya kweli, nayo ajalie

Baba ooh baba ooh, daddy ooh(Baba)
Najua una hamu sana, mwana
Ndoa ooh, ndoa oooh, ndoa oooh
Ya mi mwanao kuiona

Kaza roho, kaza roho
Dua njema atajibu Maulana
Mke mwema aaah
Atakuja baba

Chorus

Ayee, ndoa eeh, Nuia baba
Sijamuona wa kuoa eeeh, Utaoa mwanangu
Ayee, ndoa eeh, Nuia baba
Sijamuona wa kuoa eeeh

Verse Two

Ng’aa tena dafaradhi
Kumhalalisha mwanangu
Kwangu mimi ni heshima
Nikimwona mkwe wangu

Kudanga danga si kwema
Kwa leta laana mwanangu
Leo Ali kesho Juma
Hebu tunza utu wako

Mama wakitongoza
Wanataka kuvua na nguo
Ah tumejuana leo
Anataka kunivua nguo eeh

Wanaume wa sasa
Suruali kushuka eeh
Mama niombee kwa Mungu
Nipate mwema niweze sitirika

Leta mjukuu nilee
Aje anikojolee
Ooooh, ooooh

Mama ooh mama ooh, mama ooh
Najua una hamu sana
Ndoa ooh, ndoa oooh, ndoa oooh
Ya mi mwanao kuiona

Kaza roho, kaza roho
Dua njema atajibu Maulana
Mume mwema aaah
Atakuja tu mama

Chorus

Ayee, ndoa eeh, Nuia mwana aah
Sijamuona wa kunioa eeeh
Ayee, ndoa eeh
Sijamuona wa kunioa
Sijamuona wa kunioa eeeh

I say mama ma, mama
Ayee, ndoa eeh
Sijamuona wa kunioa
Sijamuona wa kunioa eeeh

Utampata baba ano kuridhia
Nataka nicheze eeh, mwanangu
Siku hiyo wanione eeh, mwanangu eeh
Nikate, nikate, kwa furaha yangu wee eeh

Ndoa Lyrics Credit – Bright, Khadija Kopa, Juma Kakere and Karen

ALSO, SING TO – Naolewa Lyrics – Ruby – New Song Feb 2020