Home HEALTH NCHI TANO ZA AFRIKA ZIKO MBIONI KUMALIZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

NCHI TANO ZA AFRIKA ZIKO MBIONI KUMALIZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

0

 

Huku dunia ikiwa mbioni kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030, mara tu programu muhimu za afya zitakapofadhiliwa kikamilifu, ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema, eneo la afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako asilimia 65 ya watu wote wenye VVU wanaishi, linapiga hatua kubwa katika kumaliza ugonjwa huo.

 

Kati ya inchi hizo ni Botswana, Eswatini, Rwanda, Tanzania na Zimbabwe tayari zimefikia lengo la asilimia 95 kwa mujibu wa ripoti ya UNAIDS.Hii ina maana kuwa, asilimia hiyo ya watu wanaoishi na Virusi hivyo, wanajua hali zao za kiafya, huku wanaojua hali zao wameanza kupata matibabu ya kurefusha maisha.

 

Hata hivyo idadi ya watu hao wanaopata matibabu wamevifubaza virusi hivyo, na hivyo basi kuna uwezekano wa wao kutoweza kusambaza na kueneza virusi hivyo kamwe.Mataifa mengine 16, nane kati yao katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara pia yanakaribia kufikia lengo hilo.

 

Hata hivyo Winnie alidokeza kuwa endapo idadi hiyo itaendelea kupata matibabu hayo basi kunauwezekano wa wao kwa ushirikiano na shirika hilo kusaidia pakubwa kuokoa mamilioni ya maisha na kulinda afya ya kila mtu na kuonesha kile ambacho uongozi wa shirika hilo unaweza kufanya.

Ingawaje UNAIDS inakabiliwa na upungufu wa dola bilioni 8.5 katika bajeti yake kwa nchi za kipato cha chini na cha kati ifikapo mwaka 2025 ila shirika hilo limesema kuwa maendeleo hayo yangeweza kuharibiwa kwa urahisi iwapo mtu mmoja angefariki kila dakika kutokana na Ukimwi mwaka 2022 kama matibabu hayo hayange vumbuliwa.

 

Lakini bado kuna vikwazo vya kushinda kila wiki, wasichana na wanawake 4,000 wanaambukizwa Virusi hivyo kila uchao.Na katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, licha ya maendeleo, Umoja wa Mataifa unasema wanawake na wasichana wa rika zote walichangia asilimia 63 ya maambukizi mapya ya Virusi mwaka 2022.

 

Jaribio la chanjo ya VVU linaendelea nchini Uganda, Tanzania na Afrika Kusini ambalo linachanganya chanjo za majaribio za VVU na za pre-exposure prophylaxis (PrEP) kwa wakati mmoja, jambo ambalo halijawahi kufanywa hapo awali.Nchini Botswana kusini mwa Afrika, wasichana wanasalia katika hatari ambapo wanaume wazee huwawinda, inayojulikana kama ‘ngono kati ya vizazi’