NAY WA MITEGO YU TAABANI | ATAKIWA KURIPOTI BASATA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtaka msanii ‘Nay wa Mitego’ kufika kwenye ofisi za Baraza hilo leo na sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kutokana na wimbo wake mpya wa ‘Amkeni.’
Nay, amethibitisha kupokea barua hiyo lakini ameomba siku nyingine ya kuweza kufika kwenye ofisi za Baraza hilo kwasababu kwasasa yupo safarini.
“Nimepokea Barua Ya Wito Leo Asubuhi Kutoka baraza La Sanaa Tanzania #Basata Ikiniitaji Kufika Ofisi Za Basata Leo Saa Nne Asubuhi. Isue Ni Wimbo Wangu Wa #Amkeni
Nimeshindwa Kufika Leo Coz Nipo Safarini, Mwanasheria Wangu Amesha fanya Mawasiliano Nao Kuomba Siku Nyingine” Msanii Nay wa Mitego
Kwenye wimbo wake mpya AMKENI, Ney anaimba,
“Nchi Inaendeshwa Kwa Magendo Mama Yenu Anafuga Wezi Bandari Kauziwa warabu, Mungu Kwanini Ulimchukua John Pombe Mapema? Ulimchukua Ili Tujifunze Au Tupate Kupumua?”
Hiyo ni mistari kutoka kwenye Wimbo Mpya wa Nay wa Mitego