Mwanaharakati wa haki za binadamu Boniface Mwangi amemkosoa Jaji Mkuu Martha Koome kwa tabia yake. Mwangi alisema kuwa Jaji Mkuu Martha Koome anastahili kulaumiwa kwa kesi kuchukua muda mrefu mahakamani bila sababu thabiti.
Akizungumza siku ya Ijumaa,wiki iliyopita nje ya Mahakama ya Milimani, yeye kama “mwangalizi wa watu” alisema kuwa Koome hapatikani mara nyingi kutekeleza majukumu yake. Mwangi alisema kuwa tabia hiyo inaathiri maafisa na wafanyakazi wengine wa mahakama chini yake, na kuwaeleza kuwa watu hukaa mahakamani kwa masaa mengi wakisubiri majaji na mahakimu ambao wakati huo hawajulikani waliko.