Home GENERAL Mungu Yuko Wapi Lyrics Nay Wa Mitego Ft Shamy

Mungu Yuko Wapi Lyrics Nay Wa Mitego Ft Shamy

0
Mungu Yuko Wapi Lyrics

Mungu Yuko Wapi Lyrics Nay Wa Mitego Ft Shamy.

Nilizaliwa peke yangu
Na nitakufa peke yangu
Muamini Mungu wako
Nibaki na Imani yangu

Kama kweli kuna mbingu
Basi nina njia yangu
Sio baba sio mama
Nitakwenda peke yangu

Mungu hamtupi mja wake
Imeandikwa kwenye vitabu
Mbona Shetani ametawala
Na waja wanapata tabu

Hivi kweli huyu Mungu yupo?
Na huu mchafuko
Uliyokataza yametawala
Hivi kweli we Mungu upo?

Wenye roho mbaya
Mungu ni wewe umewapa hela
Wana makosa kibao
Na bado hatuwaoni jela

Kuna hawa viongozi makatili na madikteta
Wanatesa watu wanauwa watu
Sababu ya madaraka wanajiona Miungu watu

Baya zaidi hawafi haraka
Watu wenye roho mbaya
Mungu ni kweli upo
Na unayatazama haya

Hivi ni wewee, ni wewee
Hivi ni wewee
Asa mbona upo kimya

Hivi Mungu yuko wapi
Hivi Mungu yuko wapi
Hivi kweli Mungu yupo
Hivi kweli Mungu yupo

Ninae muabudu mimi
Sio mnaemuamini nyinyi
Najua tuko tofauti
Kuanzia imani mpaka dini

Na sitoshangaa
Msipoelewa naongea nini
Maana mi mwenyewe sielewi
Mnashangaa nini

Pumbavu nyinyi wajinga nini
Mnateswa mnanyanyaswa
Mnangoja niseme mimi
Eeh Mungu baba hivi kweli unawaona

Hivi anaewapa hela mashoga ni Mungu gani
Wanaosagana wana roho gani ya imani
Mbona dada yangu ameokoka ila anakufa maskini
Wakati wenzake wadangaji anawapa hela kwa nini

Au ushakula kona shetani ametake over
Manabii wa uongo wamejaa kila sehemu
Tunalewa nao tunashare nao mademu
Sadaka za watu wako ndo zinawapa wazimu

Wanaa jina lako wanaponya kwa nguvu za giza
Ufuska mauaji ukatili uliopitiliza
Hivi kweli mungu upo
Ndo swali nnalojiuliza

Hivi ni wewee, ni wewee
Hivi ni wewee
Asa mbona upo kimya

Hivi Mungu yuko wapi
Hivi Mungu yuko wapi
Hivi kweli Mungu yupo
Hivi kweli Mungu yupo

Wanaokesha kwa waganga
Wanafanikiwa kwa spidi
Wanaokesha kwenye ibada ndio
Hivi kweli mungu upo
Na unayaona haya

Hivi ni wewee
Hivi ni wewee, ni wewee
Hivi ni wewee,
Asa mbona upo kimya

Tanzania Ya Sasa Lyrics Zuchu

Mungu Yuko Wapi Lyrics Nay Wa Mitego Ft Shamy – Download Mp3 Audio

Previous articleTanzania Ya Sasa Lyrics Zuchu
Next articleSafaricom Jitambulishe Service. How to Enroll, How to use Jitambulishe, How to De-enroll