Mauzauza Lyrics by Zuchu and Khadija Kopa – Download Mp3 Audio
Mauzauza Lyrics Verse One
Mocco
Funua usijipe mapana
Eti mwili kujitutumusha
Nitakutawanya
Ka bahari na fimbo ya Musa
Umejigeuza soji
Si wa Corolla wala Vogi
Na hilo wala kufoji
Eti lina kupa kodi
Oooh leo nikome Mwenye kiranga Mwenye Kiranga
Hujalijua vizuri litimbwi ni la vanga Mwenye kiranga
Oooh leo boda umeyabana ka Mwenye kiranga
Mi maskini jeuri sitegemei madanga, Mwenye kiranga
Chorus
Mauzauza we mwana mauzauza
Si wamekushindwa kwenu
Walimwengu tutakufunza
Mauzauza we mwana mauzauza
Si wamekushindwa kwenu
Walimwengu tutakufunza
Verse TwoÂ
Unani ni kichwa cha chikichi
Umevaa kinu unatwangia mchi aah
Mwali kigego mwenye nyota ya mitara
Hivi kungwi wako nani wewe? Atajijua
Uso mitego imedoda biashara
Hueleweki si kunguru si mwewe
Wadala ubaki dala mwenzio mimi kibunja
Haufai kwa kafara si puzi wewe ni punja
Umejivesha ubezezi kwa mapana na marefu
Uso na kazi si wa ndala wala peku
Ooooh ondoa ndo mlezi wa hana
We ebu ndege zoa zoa’
Mwali pengo binti mwanya
Tuchunge kwa kudonyoa
Oooh leo nikome Mwenye kiranga, Mwenye Kiranga
Hujalijua vizuri litimbwi ni la vanga Mwenye kiranga
Oooh leo boda umeyabana ka Mwenye kiranga
Mi maskini jeuri sitegemei madanga, Mwenye kiranga
Chorus
Mauzauza we mwana mauzauza
Si wamekushindwa kwenu
Walimwengu tutakufunza
Mauzauza we mwana mauzauza
Si wamekushindwa kwenu
Walimwengu tutakufunza
Mauzauza Lyrics Verse Three
Hahaa kuvaa dera si kazi,
kazi kulikamatia eeh
Utayaweza yangu, yako yanakushinda
Utayaweza yangu, yako yanakushinda
Ooooh tikisa ndole
Utayaweza yangu, yako yanakushinda
Uso kasi mwana wako
Utayaweza yangu, yako yanakushinda
Oooh…nadilidadi
Utayaweza yangu, yako yanakushinda
Usonoga kwa chumvi wala magadi
Utayaweza yangu, yako yanakushinda
Mauzauza Lyrics by Zuchu and Khadija Kopa
ALSO, SING TO – Ashua Lyrics – Zuchu Ft Mbosso