Home NEWS MAUMIVU YA JARIBU LYRICS – MARTHA MWAIPAJA

MAUMIVU YA JARIBU LYRICS – MARTHA MWAIPAJA

0
MAUMIVU YA JARIBU LYRICS

MAUMIVU YA JARIBU LYRICS BY MARTHA MWAIPAJA

Eee Yesu wangu

Japo jaribu
Limeruhusiwa na wewe Mungu
Hili jaribu, linaumiza moyo

Japo jaribu
Limeruhusiwa na wewe Mwenyewe
Hili jaribu, linatesa moyo

Japo maumivu haya
Yesu wayajua
Moyo wangu unateseka

Japo haya yote
Wewe pekee wajua
Lakini moyo wangu
Unatesekaa

Naishi katikati ya watu
Wasiojua ni nini napitia
Natembea katikati ya watu
Wasiojua maumivu yangu

Kwa sababu ya mateso niliyonayo
Nimejaribu kuelezea wengi
Pamoja na kuwaeleza
Bado hawajaelewa ninavyoteseka

Nilijuwa kwa kuwaeleza kwangu
Watajuwa nitesekavyo
Hawakujuwaa

Japo maumivu haya
Wewe Yesu wayajua
Lakini moyo unatesekaa

Naomba kwa unyenyekevu
Usiniache jaribuni
Kanimezaa

Baba yangu mimi nimekubali kupita
Lakini, usiniachee
Nimekubali kupitia
Usiniache nikamezwa na jaribu

Japo Ibrahimu
Aliitwa baba wa Imani
Moyo wake ulitesekaa

Japo Ibrahimu
Ulisema naye
Ukamwambia utampa watoto
Bado alilia

Pamoja na kwamba
Ulisema nae mwenyewe
Alipochelewa Isaka
Ibrahimu kalia

Japo alijuwa
Ni wewe baba utampatia
Ibrahimu moyo uliuma

Kwa sababu Ibrahimu
Alichelewa kupata mtoto
Moyo wake uliteseka

Japo alijuwa
Isaka ni mtoto wa pekee
Kwa sababu alichelewa alilia

Alijuwa, utampa watoto wazuri
Lakini moyo wa Ibrahimu
Ulilia

Pamoja na kwamba unatufundisha
Majaribu lazima
Lakini mioyo inauma

Usituache Yesu Usituache Wanao
Usituache wanao
Tukapotea

Usituache Baba Usituache we baba
Usituache wanao
Tukaangamia

Oooooh
Usituache Yesu Usituache Baba
Usituache wanao
Tukapotea

Pigania Yesu
Usituache Yesu Usituache Baba
Usituache wanao
Tukapotea

Jaribu linatesa
Usituache Yesu Usituache Baba
Usituache wanao
Tukapotea

Tusimezwe na jaribu
Usituache Yesu Usituache Baba
Usituache wanao
Tukapotea

Nena na Sisi Yesu
Usituache Yesu Usituache Baba
Usituache wanao
Tukapotea

Vita ni kali sana
Usituache Yesu Usituache Baba
Usituache wanao
Tukapotea

Eeeeh Baba
Usituache Yesu Usituache Baba
Usituache wanao
Tukapotea

Usiache Wababa
Usituache Yesu Usituache Baba
Usituache wanao
Tukapotea

MAUMIVU YA JARIBU LYRICS BY MARTHA MWAIPAJA

FOLLOW MARTHA MWAIPAJA ON YOUTUBE

ALSO, SING TO, WAGENI LYRICS – PAUL CLEMENT

Leave a Reply