Home NEWS Kwaru Lyrics – Zuchu

Kwaru Lyrics – Zuchu

0
Kwaru Lyrics

Kwaru Lyrics by Zuchu – Download Mp3 Audio

Kwaru Lyrics Verse One

Ayolizer

Mm aaah aah,
Mmm aaah
Aaaah, aah

Roho ingekuwa na macho ungejionea
Moyo haufanyi kificho ukiotea
Mimi kifigiso nacho ungeongea
Mwili wangu rojorojo nanyong’onyea

Chungu nilichopika
wamepakua wenzangu
Huruma napokutishwa
wamechukua wezangu

Na kitabu chetu cha mapenzi
Kurasa wamechanachana
Hazisomeki tena tenzi
Vimepoteza maana

Mpofu moyo wangu
Ulishindwa ona
Hukuandikwa wa kwangu
Limenikaba nalitema

Chorus

Kwaru kwa kwaru kwaru
Kachukua kisu ye anaukwarua
Kwaru kwa kwaru kwaru
Moyo wangu unaumia

Kwaru kwa kwaru kwaru
Ye kwa nguvu anaukwarua
Kwaru kwa kwaru kwaru
Jamani moyo wangu unaumia

Kwaru Lyrics Verse Two

Eee langu tatizo
Nachuna najimaliza
Mi nakesha kumwaza
Naweweseka lake jina, ooh jina

Oooh basi kwa unyonge
Najikaza niache kulia
Maana kwake bahati sina, ooh sina

Maumivu ameipora furaha yangu
Uuuh amekwenda nayo
Na zangu mbivu zimeniozea
Hasara kwangu, oooh yatapita hayo

Mpofu moyo wangu
Ulishindwa ona
Hukuandikwa wa kwangu
Limenikaba nalitema

Chorus

Kwaru kwa kwaru kwaru
Kachukua kisu ye anaukwarua
Kwaru kwa kwaru kwaru
Moyo wangu unaumia

Kwaru kwa kwaru kwaru
Ye kwa nguvu anaukwarua
Kwaru kwa kwaru kwaru
Jamani moyo wangu unaumia

Kwaru Lyrics by Zuchu

ALSO, SING TO – Nisamehe Lyrics – Zuchu

Previous articleNisamehe Lyrics – Zuchu
Next articlePandemik Lyrics – Ochungulo Family