Kiongozi wz azimio la umoja Raila Odinga alisitisha mukutano wake uliokuwa umepangwa kufanyika hapo jana katika uwanja wa kihistoria wa Kamkumkunji akidai kuwa chama chake kilipokea taarifa za kijasusi kuwa kuna wahuni waliokuwa wamelipwa kuharibu mkutano huo.
Hata hivyo, Raila alisema kuwa chama tawala cha kenya kwanza
kilikuwa na nia ya kusafirisha makundi ya wahuni hao kutoka sehemu tofauti kuharibu mkutano huo.
Kiongozi huyo pia alielezea kuwa kikosi chake kilivamiwa na maafisa wa polisi kwa kupigwa risasi katika musafara wao wa maandamano huku wengine wakikamatwa.
“Alisema baadhi walikamatwa na maafisa wa polisi kwa kutumia vitoa machozi na maji kwa kuwafurusha katika ukumbi huo walipokuwa wamekongamana kungojea mkutano kuanza”
Vilevile kiongozi huyo alinyooshea kidole cha lawama kwa idara ya
usalama kwa kutumia nguvu kupita kiasi ambapo kiasi cha mali
isiyojulikana iliweza kuharibiwa katika maandamano hayo.
Kiongozi huyo alijitetea kuwa nia yake kuu katika kuandaa mkutano huo nikusaidia wakenya katika kushukisha gharama ya maisha kwani mswada uliopitishwa wa kifedha endapo utaanza kutekelezwa basi wakenya wengi ambao hawajiwezi wataumia.
Alidokeza kuwa serikali ya kenya kwanza iko na wajibu wakuangalia pande zote mbili kwani sauti ya wakenya wengi wameweza kulalamikia sharia hiyo hivyo basi haina budi ila kukubali waziwazi kufuta sharia hiyo na kuja na hatua zingine mpya za kupunguza gharama ya maisha.