Home BUSINESS kilio kisichosikika cha wafanyikazi cha kukatwa 3% ya Mishahara Yao Kuchangia Hazina...

kilio kisichosikika cha wafanyikazi cha kukatwa 3% ya Mishahara Yao Kuchangia Hazina ya Nyumba

0

Wembe ni uleule kwani serikali imeanza kuwanyoa wakenya baada ya kutangaza kuwa wafanyakazi wanaopokea mishahara kila mwezi watalipia makato ya nyumba kuanzia Julai 1, 2023, baada ya mahakama kuruhusu utekelezaji wa Ushuru (KRA)

Wafanyabiashara wadogo pia wamejipata pabaya baada ya kupata pigo kwani Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) itaanza kukusanya ushuru wa asilimia tatu ya pato kuanzia Julai 1.Uamuzi wa serikali, kupitia Idara ya Makazi, wa kukusanya makato ya nyumba kuanzia Julai mosi unamaanisha wafanyakazi watakatwa ushuru maradufu mwezi huu.Kwa hivyo, mishahara ya wafanyakazi wote nchini itapungua kwa asilimia tatu, ikizingatiwa kuwa ada ya nyumba ni asilimia 1.5 ya mshahara wa mfanyakazi.

Kulingana na notisi iliyochapishwa magazetini jana, Idara ya Nyumba chini ya Wizara ya Ardhi, Ujenzi, Makazi na Ustawishaji wa Miji, iliwaarifu wafanyakazi na waajiri kuwa utekelezaji wa ushuru utaanza Julai 1, 2023.Hii ina maana kuwa mfanyakazi anayepokea mshahara wa Sh20,000 kwa mwezi atatozwa Sh300 kila mwezi, pesa zitakazohifadhiwa katika Hazina ya Nyumba. Mwishoni mwa mwezi huu mshahara wa mfanyakazi kama huyo utapungua kwa Sh600.

Naye mfanyakazi anayepokea mshahara wa Sh50,000 ‘atapoteza’ Sh3,000 mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti huku wale wanaopokea Sh500,000 wakikatwa Sh15,000 zaidi kama ushuru wa nyumba, kwa miezi ya Julai na Agosti.Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Zacharia Njeru inasisitiza kuwa pesa hizo za nyumba sharti ziwasilishwe na waajiri kwa mamlaka ya KRA angalau siku tisa baada ya kukamilika kwa mwezi ambao zinapaswa kulipwa.

Kulingana na Sheria hiyo ya Fedha, mwajiri atakayekosa kuwasilisha ada ya nyumba kwa KRA atatozwa faini ambayo ni sawa na asilimia mbili ya pesa ambazo mwajiri huyo atakuwa amekosa kuwasilisha kwa mamlaka hiyo kila mwezi.Wakili Soyianka Lempaa anasema kuwa ni sawa kwa serikali kuanzisha utekelezaji wa sheria hiyo Julai 1 kwa sababu hiyo ndiyo tarehe iliyowekwa na bunge.Lakini wakili huyo anaongeza kuwa kwa maoni yake, sheria hiyo inakiuka vipengele fulani vya katiba.

Seneta wa Busia Okiya Omtata alikuwa amewasilisha kesi katika Mahakama Kuu akipinga sheria hiyo kupitishwa bungeni mwezi Juni. Jaji Muruge Thande alisitisha, kwa muda, utekelezaji wa sheria hiyo, hali iliyotoa afueni ya muda kwa Wakenya.Lakini Julai 28, Mahakama ya Rufaa iliondoa amri hiyo na kutoa nafasi kwa utekelezaji wa sheria hiyo hadi kesi ya Bw Omtatah itakaposikizwa na kuamuliwa.

Wakati huo huo, wafanyakazi wanaolipwa mshahara wa kati ya Sh500,000 kila mwezi na Sh800,000, wataanza kutozwa ushuru wa mshahara (PAYE) wa asilimia 32.5 kuanzia mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti.Kwa upande mwingine, wafanyakazi wanaopokea Sh800,000 kwenda juu watakuwa wakilipa PAYE ya asilimia 35. Chini ya sheria ya zamani wafanyakazi wote wamekuwa wakilipa PAYE ya asilimia 30.

Wafanyabiashara wadogo ambao hupata faida ya Sh1 milioni hadi Sh25 milioni kwa mwaka pia wataanza kulipa ushuru wa asilimia tatu. Wafanyabiashara wanaopata Sh1 milioni hadi Sh50m kwa mwaka wamekuwa wakilipa asilimia moja.Hatua hii itapunguza zaidi mapato ya Wakenya wakati huu ambapo wengi wao pia wanaathirika na kupanda kwa gharama ya maisha.

Previous articleHow Kenyan women expose their bodies at night on Tiktok
Next articleSaudi yaongoza kwa vifo vya wahamiaji wa Kenya katika Ghuba, anasema Waziri wa Kazi