Home NEWS Kibera Girls Na Soccer Assassins Vitani Kutafuta Mshindi Wa Divisheni Ya Kwanza

Kibera Girls Na Soccer Assassins Vitani Kutafuta Mshindi Wa Divisheni Ya Kwanza

0

Kibera Girls na Soccer Assassins vitani kutafuta mshindi wa Divisheni ya  Kwanza – Taifa Leo

KIBERA Girls Soccer watashuka dimbani Jumapili dhidi ya Soccer Assassins katika mechi ya kutafuta mshindi wa jumla wa Ligi ya Wanawake ya Divisheni ya Kwanza katika uwanja wa RVIST, Kaunti ya Nakuru.

Kibera ilimaliza kileleni mwa Zoni A kwa alama 59 huku Assassins ikimaliza kidedea Zoni B kwa kuzoa alama 46.Katika mechi nyingine ya mchujo katika uwanja uo huo, Uweza Women ya Zoni A na Bungoma Queens ya Zoni B zitamenyana katika pambano la kutafuta nafasi ya tatu.Kocha msaidizi wa Bungoma Jairus Misiko atachukua nafasi ya kocha Robert Majio ambaye anaugua.Timu hizo mbili zitakutana kwa mara ya kwanza tangu zijiunge na ligi hiyo.

Timu itakayoshinda itakuwa ya tatu kupandishwa daraja moja kwa moja hadi Ligi Kuu ya Wanawake ya Kenya (KWPL) kuchukua nafasi za Kangemi Ladies, Kisumu All Starlets na Kangemi Ladies ambazo zilishuka daraja msimu jana.Kibera walimaliza katika nafasi ya tatu katika Kombe la Wanawake la Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo mnamo tarehe 4 mwezi wa sita mwaka huu. Waliilaza Kisumu All Starlets kwa mabao 4-2 na kutunukiwa nishani ya Shaba na Shilingi150,000.

Timu hiyo ilipata tiketi ya kujiunga na KWPL msimu wa mwaka wa 2021/22 lakini ligi hiyo ikatangazwa kubatilishwa na Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF).Kibera na Assassins watarejea nyumbani na kitita cha Shilingi 500,000 kila mmoja. Mshindi wa jumla wa ligi atatunukiwa kombe kwa hisani ya FKF.Timu 15 tayari zimeshuka daraja kutoka Daraja la Kwanza katika msimu uliomalizika hivi punde.

 

Previous articleHaifai Kuweka Shule Za Chekechea Pamoja Na Zile Za Msingi
Next articleAUDIO | JZyNO ft. Lasmid – Butta My Bread| download mp3