Home NEWS Kenya ikitajwa kuongoza katika orodha ya nchi karimu zaidi katika kanda ya...

Kenya ikitajwa kuongoza katika orodha ya nchi karimu zaidi katika kanda ya Bara Afrika

0

Watu katika baadhi ya nchi maskini zaidi na zenye matatizo duniani wameonekana kuwa watu wa kutoa misaada zaidi.

Wakfu wa World Giving Index imesema Raia wa Indonesia,Ukraine na Kenya wana uwezekano mkubwa wa kuchangia misaada, kusaidia mgeni au kujitolea kwa wakati wao.

Raia wa Uingereza ni miongoni mwa wanaochangia fedha nyingi zaidi lakini hawakotayari kusaidia watu ambao hawafahamu.

Indonesia ndilo taifa ambalo linakisiwa kuwa watu wakarimu zaidi duniani, wakati inapokuja suala la kutoa na kuchangia Misaada. Hii ni kwa mujibu wa wakfu wa kutoa misaada ya kibinadam wa he Charities Aid Foundation (CAF).

Ripoti hiyo ya CAF inayoratibu mpango wa uchangishaji kwa ajili ya misaada, ni moja ya utafiti wa kina uliowahi kutolewa, huku mamilioni ya watu wakihojiwa kote duniani tangu mwaka wa 2009.

Uchunguzi wa mwaka huu ulikusanya maoni kutoka kwa nchi mia moja arubaini na mbili duniani ambako watu waliuzwa maswali matatu.

La kwanza ikiwa je umewahi kumsaidia mgeni? umewahi kumpa fedha mgeni na swali la tatu ni je umewahi kujitolea kumsaidia mgeni katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita?

Licha ya kuwa raia wa taifa la Uingereza ndio wanaochangia zaidi, harakati za kutoa misaada hasa fedha, taifa hilo limeshuka hadi nafasi ya hamsini na nane katika orodha ya mataifa ambayo raia wake wanajitolea kwa kazi za hiari na pia kushuka hadi nafasi ya 112 katika orodho ya nchi ambazo raia wake wanaweza kumsaidia mgeni.

Mataifa yaliyopanda tena hadi nafasi kumi bora

Katika orodha ya nchi karimu zaidi katika kanda ya afrika, Kenya inaongoza huku iikishikilia nafasi ya tatu duniani ikifuatwa na Liberia na Nigeria.

Leave a Reply