Kiwanda cha maziwa cha Brookside Limited kinachomilikiwa na familia ya Kenyatta kimejipata pabaya na kuwa futa nusu ya wafanyakazi wake nchini Uganda kutokana na kupungua kwa thamani ya bidhaa zake zilizoagizwa nchini Kenya. Katika barua hiyo, kampuni ilielezea kushindwa kwa serikali ya Kenya kutoa kibali cha kuuza nje bidhaa kama vile cream, siagi, mtindi, samli, na unga wa maziwa kwenda Nairobi. Barua hiyo ilikuwa imeandikwa kwa kamishena wa kazi wa Uganda katika Wizara ya Jinsia, Kazi na Maendeleo ya Jamii.
Meneja wa rasilimali watu wa Brookside, Winnie Mirembe Mugabi, alifichua kwamba kutofanikiwa kupata kibali tangu mwezi wa tatu mwaka huu kulizuia Brookside Uganda kupata fursa ya kufikia asilimia 75 ya soko lake nchini Kenya. Meneja Rasilimali watu alieleza walichukua hatua kali ya kusitisha mikataba ya wafanyakazi kutokana na sababu za kimuundo.
Vyombo vya habari viliripoti kwamba Brookside Uganda ilijaribu bila mafanikio katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuweka wino kwenye dili lakini ikashindikana.Kwa sababu hiyo, haikuwa na budi ila kuachisha kazi nusu ya wafanyakazi wake.