Tume ya kuwapanga Watahiniwa katika Vyuo na Vyuo Vikuu nchini Kenya (KUCCPS) imetangaza kuwa wanafunzi sasa wataweza kuangalia matokeo ya upangaji kupitia tovuti yao.Kupitia taarifa ya Jumatatu asubuhi katika ukurasa wake wa Twitter , KUCCPS ilisema kwamba wanafunzi pia watapata kujua chuo kikuu walichochaguliwa kujiunga nacho kwa kutuma SMS kwa nambari 20842.
Watahiniwa watatuma index number zao kuanzia mwaka waliomaliza mtihani wa KCSE.Hata hivyo, walibainisha kuwa mtu atagharamika wakati wa kutuma SMS hiyo.Iwapo kutatokea shida au ugumu wowote, KUCCPS ilibainisha zaidi kwamba mtu anaweza kufikia nambari yao ya usaidizi ya 020513740 ili kusaidiwa.
Waziri Elimu Ezekiel Machogu Jumatatu alitangaza kwamba watahiniwa wa KCSE waliofanya mtihani wao mwaka jana sasa watajua vyuo vikuu walivyopangiwa.Alisema kozi zote zinazopatikana katika taasisi hizo zinafadhiliwa na serikali kuambatana na mfumo mpya wa ufadhili wa chuo kikuu na TVETs uliozinduliwa na Rais William Ruto mnamo Mei 3,huku Kiwango cha chini cha kuingia katika chuo kikuu ni C+.