Grow Up Lyrics – Nacha – Download Mp3 Audio
I go by the name N.A.C.H.A aka Nacha
Mnyasubi ndani ya mbanyu beiby
Asante Mungu kwa kunipa pumzi ambayo silipii ushuru
Nisipokushukuru ni dhahiri moja kwa moja nakukufuru
Asante kwa kunipa nafasi ya kuongea na wanao nisikiliza
Ili nijue kama wamekuwa ama wanahitaji kumwagiliziwa mbolea ili kukua
Tunahitaji kugrow up maana tuna akili finyu kwa kuwa
Tunaweza kulipia hoteli elfu hamsini
Kufanya sex alafu condom ni ya mia tano tu
Ikatushinda kununua, nobody care, grow up
Ajira zimekuwa ngumu, kaka yangu kahitimu chuo kikuu cha Dar es Salaam
Kaamua kujikita kwenye michezo ya kubahatisha
Swali ni je? Kubet ndio kitu alichosomea kutoka Standard One mpaka chuo?
Grow up aisee wavalisheni nguo
Mi huwanga sichukuliangi vitu personal though
Kuna mtangazaji aliyesema kumpa Nacha interview ni mpaka awe na demand mtaani
Question hiyo demand nitaipata vipi wakati nahitaji kusupportiwa ili niwe na hiyo demand mtaani
Yaani ni sawa na mtu kutoka chuo na kuomba kazi
Alafu unamwambia ni lazima awe na uzoefu wa hiyo kazi, nonsense….
Sababu za kiinteljisia utapasuka msamba ukijaribu kuwa iga
Na ukijaribu kuupaza sauti na kuwauliza kwa nini nyinyi mnakula vya juu
Watakujibu tunakula vya juu sababu tuna shingo za twiga
Phhhw huo ni ubinafsi ulafi na uchoyo wa kutaka wao pekee yao
Na ndugu zao mikono yao iende kinywani alafu mikono yako iende shavuni
Take care grow up
Bado nawashangaa wadau wa kandanda bongo
kwa kukiponda chama cha mpira cha nchi hii kwa ovyo
Eti national team haijafuzu world cup ama AFCON
Nina swali nataka majibu sio kingine
Serikali inasupporti soka kama sekta nyeti zingine
Je tuna waalimu wenye taluma na leseni za juu kutoka FIFA
Na je shuleni michezo ni lazima kwa maana umeitashume tena ni setup
Na mwisho kabisa nchi yako ina viwanja bora na academy za kutosha
Big no definitely
Mafanikio ya chochote ni maandalizi toka chini
Acheni kuchekesha grow up
Nilichoamua ni kumwamini mungu tu ila kumwamini mwanadamu mwenzangu sitaki
Tena huo ni unafiki Mtumishi wa mungu kutufundisha mema huku kwa simu yake kajaza pornography
Wizi grow up , Mnadhani nawahofia? hapana msichokijua ni kuwa nahofia Anopheles
Ndio maana kabla ya kulala nakishukisha chandarua
Na nangoja tu niwajuze, wa kumsimamisha roma sio stamina
Ni napoli, inter milan au Juve trust me
Kibaya ni kuwa tumezaliwa kwenye nchi ambayo wasomi wako mtaani
Ndio maana mi niliamua tu kuingia madrasa kuhifadhi Bible na Qurani
Kizazi cha four kizazi cha instagram, kizazi cha facebook, Kizazi cha WhatsApp
Kizazi cha Twitter, Kizazi cha Telegram, Kizazi cha Smartphone,
Make up na fashion za kim kardashian na Migos ndio kizazi cha vigoma
Na ndio kizazi cha zero nadhani wotee mnakiona na
ndio maana kila siku tutazidi kuzalisha akina Amber Ruty wengi
Tena under age kuitaka ndoa wakati huwezi kumpikia hata mume Uji
Muungwana humpongeza muungwana akifanya vya maana
Watumishi hewa walifyekwa safi barabara safi treni ya mwendo kasi na fly over
Bado tu serikali ya viwanda, ajira kwa vijana, kupanda mishahara kwa walimu na polisi
Ndio vitu ninavyoongoja
Tumeitupa Bongo fleva na kuiga soundi ya nigeria
Au mi ndo sijajuwa pengine bongo fleva is a type of nigerian music
I don’t know, mpaka sasa mtaani ni msoto na sijakutana na what is biology?
Mpaka naamini huo ni uzushi labda study za kazi kidogo imenisaidia kuwa fundi Washi
Bahati mbaya mi sio mwarabu sina kitu cha kurithi
Mtaniua bure babangu ni masikini , mamangu ni masikini
Na hata kwetu kijijini nilichoachiwa sio mali za ng’ombe sabini
Ila nimeachiwa utajiri kichwani kuwa this time tomorrow ni past day like a shadow
Grow up
Ubinafsi ndio kitu nilicho nyimwa nyinyi si mlizipandisha na mungu utu huyu ustadhi
Njombe mji lipuli maji maji na ndanda mimi nitazipandisha Nyasubi fc, Kahma united
Stendi united, mbang’a fc, Rhino rangers, Mtoto africans pamba na Gwambiraa
Guess what? mi sikuzaliwa nje ya ndoa la hasha ndio maana nawaheshimu sana wanawake
Ndio maana naogopa kuwachezea na kuwazalisha na kuwatelekeza na niishie kuwatia
Yaani kuwatia dosari na kuwatia doa
Asa kumbe ata iwe ni msoto iwe changamoto rijari hakatai mtoto
Mkamatwa na ngozi si ndio mula nyama asa mbona mnawahanya
Mwenyekiti wa chama tawala na mgogoro mzito na mwenyekiti wa chama pinzani
Phww jameni punguzeni ushabiki kitu haukijui unakausha
Maana sisi hasa wengi wetu hatuna uelewa kuhusu siasa
Sijajuwa ni uzembe wa mzazi uzembe wa walimu au ni mfumo wa elimu
Ndio unasababisha kumkuta mtoto wa darasa la tano hajui kusoma wala kuandika
Globalization, Mtakuwa wajinga mpaka lini kuunga megabytes kwa ajili ya kufuatilia
Udaku, picha chafu za video za sanchoka
Nagundua tunakwenda ni mbali sana kuliko tulipotoka
Grow up
Ni utandawazi au ni uzembe ulifanywa na wazazi
Sa ivi ni kawaida kumkuta kijana mwenye umri wa miaka thelathini kuishi kwa wazazi, grow up
Nawawashia green lights taifa la mbumbumbu kushadadia mambo
Na ndo maana kwwenye ngoma serious kama hizi utakuta dislikes
Kuwasaida hawa sio kuwapa laki mbili bali kuwasaidia hawa ni kuwafanyia counselling ya akili
Kabla ya kupigana kutukanana huwa nageuka nyuma najiuliza mi ni nani nimetoka wapi
Ndoto zangu zipo naweka silaha chini na kuwa mpole kwa maana
Mjini sina cha shangazi sinza wala mjomba kwa mtogole
Ako na watu sai wanajiuliza kwa nini Nacha haiti
Kwa nini Nacha hawi star na mawe yake yanapendwa sana kwa mtaa
Nawajibu mi ni mwezi kamwe siwezi kuwa star
Guess what? wanawake wa sasa ingawa sio wote ila wengi wao wana tamaa
Hawana kinyaa wanameza matapishi ambayo rafiki yake kayakataa
Na ndio maana wanazidi kuambukizana moto sababu ya motor car
Na ndio maana vijana wwengi sai wanatumia muda mwingi kujiremba kama mabinti
Kuwa smart kutafuta majimama ni true sio masihara kuliko kutumia muda mwingi kutafuta kazi wapate
ugali ili wawe wanaenda chooni mara kwa mara grow up
Asanteni naitwa Nacha
Grow Up Lyrics Credit – Nacha
ALSO, SING TO – Gere Lyrics – Tanasha Ft Diamond Platnumz – New Song 2020