Hasara Roho Lyrics by Goodluck Gozbert – Download Mp3 Audio Here
Verse One
Penda nipende nikiwa hai
Sio nikifaa
Na tena ni bora uniambie
Ukiniona
Vile unavyonisaidia
Usinitangaze
Utanisitiri bwana
Wewe
Usicheke, usicheke
Maana kesho huoni
Ya duniani ni siri
Kupita za moyoni
Tena niombee
Nami niwe na kheri
Kati ya wenye furaha
Sitokusumbuaa
Kama shillingi, shillingi
Manoti, manotii
Yaani hizo ni per DM
Zisikuchanganye
Kesho firimbi, firimbi
Kama roboti, roboti
Haya maisha ni gwaride
Yasikuchanganye
Chorus
Hasara roho, hasara roho
Hasa basi basi tukumbukane
Hasara roho, hasara roho
Hasa basi basi tukumbukane
Verse Two
Washa tabasamu
Walau kwa moja
Ibaki kwenye moyo
Usipandishe vioo
Maisha ni tofauti
Ukishiba shukuru
Ona walio wengi
Wanalia na njaa
Na kama huwezi nisaidia
Usiniumizee
Ya duniani ni siri
Kupita za moyoni
Tena niombee
Nami niwe na kheri
Kati ya wenye furaha
Sitokusumbuaa
Kama shillingi, shillingi
Manoti, manotii
Yaani hizo ni per DM
Zisikuchanganye
Kesho firimbi, firimbi
Kama roboti, roboti
Haya maisha ni gwaride
Yasikuchanganye
Chorus
Hasara roho, hasara roho
Hasa basi basi tukumbukane
Hasara roho, hasara roho
Hasa basi basi tukumbukane
Hasara Roho Lyrics by Goodluck Gozbert
ALSO, SING TO, MAUMIVU YA JARIBU LYRICS – MARTHA MWAIPAJA