Home FEATURE STORIES Familia zinalalamikia utendakazi wa shirika la IPOA huko lamu

Familia zinalalamikia utendakazi wa shirika la IPOA huko lamu

0

 

familia zinalilia haki wakidai polisi wanaua watoto wao

familia, ndugu, dada, wazazi na marafiki wa waliouawa walieleza kushangazwa kwao na jinsi shirika la IPOA linavyoendelea ‘kujikokota’ katika kutafiti na kuwachukulia hatua maafisa waliochangia maafa kwa wapendewa wao.Familia hizo zikiongea na wanahabari huko Lamu zinalalamika kuwa miezi kadhaa imepita tangu walipopatwa na mikasa ya watu wao kuuawa na polisi ilhali IPOA ikikosa kuwafikia na kuwaeleza hatua zilizopigwa katika kuchunguza dhuluma hizo.

 

Feiswal Miji, ambaye ni nduguye Aboud Miji Zambavu anayedaiwa kuuawa kwa kunyongwa na polisi waliomlazimisha kutapika dawa alizokuwa anadaiwa kumeza mnamo mwezi wanne mwaka huu, alisema licha ya mwenyekiti wa IPOA Anne Makori kufika Lamu na kuwaahidi kwamba wangepata haki ya mpendwa wao, kufikia sasa hakuna lolote ambalo wamefahamishwa.Bw Miji aliitaja IPOA kuwa kitengo kinachotumiwa vibaya kunyamazisha waliodhulumiwa kupitia matamshi matamu ilhali hakuna vitendo vyovyote.

IPOA report implicates top State officials in Lamu killings, shows frosty working relations - The Standard

Familia nyingine inayolalamikia utepetevu wa IPOA ni ile ya mama Mariam Mohammed Hilesi ambaye pia alimpoteza kijana wake Omar Hussein Shizo mapema uo huo wan nne mwaka huu.Omar alipatikana akiwa ameuawa nje ya kambi ya polisi wa BPU eneo la Kiangwe msituni Boni muda mfupi baada ya kufikishwa kambini humo kwa madai ya kuiba kilo 5 za chakula cha msaada.Bi Hilesi alisema licha ya IPOA kuahidi kuchunguza tukio hilo na wahusika kuadhibiwa, hakuna hatua yoyote kufikia sasa wamejulishwa kwamba imechukuliwa na haki kutendeka kwa familia yake.

 

Mjini Hindi, familia ya mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Mohamed Shee Omar pia imesalia bila jawabu tangu kijana wao alipopigwa risasi na kuuawa na polisi usiku wa tarehe 17 mwezi wa sita mwaka huu.Binamu wa mwendazake, Bi Baraka Athman anasema wamekuwa wakisubiri kutimizwa kwa ahadi ya IPOA kuchunguza na kuwachukulia hatua walinda usalama waliohusika na mauaji tata ya kakake.Hadi sasa hakuna hatua zozote walizofahamishwa kuhusiana na matukio hayo.

 

Afisa Mshirikishi wa Shirika la Kutetea haki za Binadamu la MUHURI, kaunti ya Lamu, Mohamed Skanda aliisisitizia IPOA kuwajibikia jukumu lao kwa kuhakikisha waliokiuka haki za binadamu, hasa polisi, wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.Katika mahojiano na wanahabari aidha, Mkurugenzi wa IPOA Ukanda wa Pwani, Hussein Aden, alikana madai kuwa IPOA haiwajibikii kazi yake.Badala yake, Bw Aden aliwataka wananchi kuzidisha imani yao kwa IPOA, akishikilia kuwa afisa yeyote wa usalama aliyekaidi amri kazini lazima achukuliwe hatua.

Previous articleOdiero JaMjengo Biography, age, education, career, family, wife, net worth
Next articleMabunge Ya Kenya Na Australia Kushirikiana Kiutendakazi pamoja