Ex Boyfriend Lyrics – Rayvanny – Download Mp3 Audio
Verse One
Leo nakula kwa macho
Nguvu ya kusema sinaa
Maneno ya mipasho
Na jeuri vimeshazimaa
Nilishafuta namba zako
Nikachoma picha zako
Sikujali ulivyoliaa
Mbele ya mashoga zako
Nikasema uende zako
Nguo nikakutupia
Na zaidi uliuguza vidonda
Kwa vipigo manyanyaso kila siku
Kwa mawazo ukakonda
Nikubize kucheat na fungwe zi
Ulinibembeleza nikakubeza
Unanuka na nikakutelekeza
Macho makengeza miguu ya pweza
Kuwa nawe nikasema niliteleza
Leo unapendeza wamekutengeneza
Wanaume wenye mali wenye fedha
Sasa unajiweza siwezi kujikweza
Najutia nafasi kuipoteza
Chorus
Leo haipo yangu,
Ex Boyfriend, Ex Boyfriend, Ex Boyfriend
Siitwi tena hunnie baby jina langu limekuwa
Ex Boyfriend, Ex Boyfriend, Ex Boyfriend
Sikujuwa kumbe tabu pekee yangu naugua
Nawaza nilifeli wapi Kusema sikutaki
Sura ya baba na kitambi cha magasi
Sa una mtanashati vitozi tena smarti
Mtu wa gym tena ana six packi
Mi nipo juu ya bati sina mikakati
Ghetto mwendo chai na chapati
We ushahama mburatii una nyumba masaki
Mnachoma nyama kila siku party
Mshanipiga mikuki, aaa
Insta mi sifurukuti, aaa
Mambo ya gauni suti, aaa
Mkifanya photo shooti, aaa
Mapenzi hayana commando
Mwenzako inaniuma roho
Natamani nikuite njoo
Turudi kama before
Kumbe shepu ilijificha kwenye dera
Hizo skinny jeans mama zina kera
Utaniletea kadi kwenye machela
Siku wakikuvalisha shela
Na Ulinibembeleza nikakubeza
Unanuka na nikakutelekeza
Macho makengeza miguu ya pweza
Kuwa nawe nikasema niliteleza
Leo unapendeza wamekutengeneza
Wanaume wenye mali wenye fedha
Sasa unajiweza na sio najikweza
Najutia nafasi kuipoteza
Chorus
Leo haipo yangu,
Ex Boyfriend, Ex Boyfriend, Ex Boyfriend
Siitwi tena hunnie baby jina langu limekuwa
Ex Boyfriend, Ex Boyfriend, Ex Boyfriend
Sikujuwa kumbe tabu pekee yangu naugua
Ex Boyfriend Lyrics Credit – Rayvanny
ALSO, SING TO – Vumilia Lyrics – Rayvanny – New Song 2020