Home NEWS Corona Lyrics – Lava Lava

Corona Lyrics – Lava Lava

0
Corona Lyrics by Lava Lava

Corona Lyrics by Lava Lava – Download Mp3 Audio

Verse One

Eh mola waja wako tumesimama
Tuonyeshe suluhisho
Kutwa tumeshika tama
Hatuishiwi masikitiko

Ama hizi ndio zile zama
Ziloandikwa za mwisho
Watoto wanalia baba mama
Wote manung’uniko

Nilidhani utani wanatudanganya
Waongo nikawaona nikawaona
Si unajua vijana wa maskani hawajuangi sana
Eti bongo hakuna Corona, coroona

Mara kitimu timu nasikia habari kila nikipita
Waziri Ummy mwalimu katangaza tayari
Kunao waathirika

Makundi kundi matimu
Tamko la serikali marufuku kukusanyika
Ukanipata wazimu nitapata wapi ugali
Show zote zimevunjika

Mmm Secondary Primary na Vyuo vyote vifungwe
Ukiona una mbaya dalili muone doctor usivunge
Ee hili gonjwa hatari hatari kabisa tujichunge
Usije ukafanya siri ,, itakuuua

Chorus

Corona, corona aaee
Unataka nini
Corona, corona aaee
Kwetu umefata nini

Corona, corona aaee
Tumekukosea nini
Corona, corona aaee
Utaondoka lini

Verse Two

Moyo umetanda hofu
Masikini mimi
Ndugu zangu walotoka Europe
Wapo Quarantine

Ishamkumba SK
Bosi wangu Salaamu
Na yule Mwana FA
Washaposti instagramu

Sorry naomba kurudia kidogo
Kipande hiki kimenihuzunisha sana

Mmm Ishamkumba SK
Bosi wangu Salaamu
Na yule Mwana FA
Washaposti instagramu

Ee na sasa wasafi kweupe
Hakuna watu ofisini
Naona marupe rupe
Jamani tuwe makini

Secondary Primary na Vyuo vyote vifungwe
Ukiona una mbaya dalili muone doctor usivunge
Ee hili gonjwa hatari hatari kabisa tujichunge
Usije ukafanya siri ,, itakuuua

Chorus

Corona, corona aaee
Unataka nini
Corona, corona aaee
Kwetu umefata nini

Corona, corona aaee
Tumekukosea nini
Corona, corona aaee
Utaondoka lini

Verse Three

Mikono kwa sabuni
Osha osha
Kwa sekunde ishirini
Osha osha

Vaa mask usilete uhuni
Osha osha
Ukiwa nyumbani ofisini
Osha osha

In God we Trust

Corona Lyrics by Lava Lava

ALSO, SING TO – Haijakaa Sawa Lyrics ā€“ Mbosso

Previous articleHaijakaa Sawa Lyrics – Mbosso
Next articleCarol Radull Biography, Career, Husband, Interview, Facts, Age