Home NEWS Azimio Wakubali Mazungumzo Ya Maridhiano Na Kenya Kwanza

Azimio Wakubali Mazungumzo Ya Maridhiano Na Kenya Kwanza

0

Siasa – Page 2 – Taifa Leo

MUUNGANO wa Azimio La Umoja-One Kenya umehiari kushirikiana na Kenya Kwanza kuunda kamati ya watu 10 kushiriki mazungumzo ya maridhiano.Kiongozi wa Wachache Bungeni Opiyo Wandayi amesema kila mrengo utakuwa na wawakilishi watano.

“Kutakuwa na wawakilishi wanne kutoka nje ya Bunge, wawili kila upande, Kiongozi wa Wengi na Kiongozi wa Wachache Bungeni kisha wabunge wanne ambapo kila upande utatoa wawili,” amesema Bw Wandayi ambaye ni Mbunge wa Ugunja.Hii ni baada ya viongozi wa Azimio kuketi chini na wenzao wa Kenya Kwanza chini ya uelekezi wa aliyekuwa Rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo kujadiliana kwa kina kuhusu mustakabali wa nchi.

Viongozi hao waliangazia umuhimu wa demokrasia na kusuluhisha maswala nyeti kwa njia ya uwazi huku wakisikitishwa na machafuko na raia kuuawa kiholela.Wamesema watatii Katiba na kusuluhisha mzozo baina ya serikali na Azimio kwa manufaa ya Wakenya.

 

 

Previous articleJinsi watahiniwa wa kcse 2022 wanaweza kuangalia chuo wamechaguliwa kujiunga nacho
Next articleNouhaila Benzina: Mwanasoka Muislamu wa kike wa kwanza kuvaa hijab mechi ya FIFA