Siku ya Usafishaji Duniani ni mpango wa kila mwaka wa hatua za kijamii wa kimataifa unaolenga kupambana na mzozo wa taka unaosimamiwa vibaya, pamoja na shida ya uchafu wa baharini. Kampeni katika ngazi ya kitaifa inaendeshwa na Kituo cha Taifa cha Mazingira (NEC).
Siku hiyo iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1993 nchini kenya huku ikiwa inalenga kukuza hatua za jamii kama ufunguo wa mabadiliko ya muda mrefu ya mazingira.
Hata hivyo mwaka huu siku hii iliadimishwa kiaina yake kote nchini huku mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yakishirikiana na serikali kudumisha siku hii.
Shirika hilo hisani la Darren Foundation lilianzishwa mwaka wa 2017 na Darren Hart, mwanafunzi wa uhandisi wa kiraia kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.Shirika hilo likiwa linashughulika na ; Uhamasishaji wa afya ya akili, utoaji wa taulo za usafi, uhifadhi wa mazingira na ushauri wa vijana katika uongozi.
Darren Hart hata hivyo, linajivunia kwa kutoa misaada na kwa jamii pia limejitolea kudumisha uendelevu wa mazingira, uwezeshaji wa jamii, na ushirikishwaji wa kijamii, kufanya kazi bila kuchoka ili kuimarisha maisha, kuhifadhi asili, na kuunda matokeo chanya ya kudumu duniani. Kupitia mipango yake mbalimbali, limehimiza huruma, limekuza kujitolea, na kumesimama kama mwanga wa matumaini, limejitahidi kujenga mustakabali bora na wenye usawa zaidi kwa wote.
Mwaka huu, kauli mbiu ya Siku ya Usafishaji Duniani ikiwa “Let’s Do It World,” kwa ajili ya kudhibiti taka ngumu na kusafisha takataka kutoka misitu, mito, mitaa na fuo.
Shirika la Darren halikuachwa nyuma kwani lilikuwa mustari wa kwanza kujitokeza katika hafla hiyo ya kufana iliyofanyika mtaani lang’ata.
Vijana kwa wazee walijitokeza kwa hali na mali katika shule ya msingi ya Uhurugarden ambapo ndio palikuwa kituo cha kwanza cha makutano kabla ya zoezi lenyewe kuanza.
Mashirika mbalimbali likiwemo Dimension Data na mashirika na vikundi vingine 45, pamoja na watu 800+ waliojitolea waliojiunga na KITOVU CHA USAFI DUNIANI.Kitendo hicho kwa ukweli kiliwavutia wakaazi wengi na wapita njia kwani shirika la Darren liliweza kujitolea vilivyo kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa utupaji taka ufaao pamoja na thamani wanayoweza kupata kwa kupanda na kustawisha miti.
Zaidi ya tani 20 za takataka ziliweza kurejesha huku miche 1000 ya miti ikipandwa katika Shule ya Msingi ya Ngei.
Kando na zoezi hilo Daren Hart foundation kwa ushirikiano na Hospitali ya Coptic iliweza kuandaa zoezi jingine la ukaguzi wa macho bila malipo, Upimaji wa HIV/AIDs na ushauri bila malipo pamoja na ushauri nasaha wa GBV ili kusaidia zoezi hilo. Zoezi hili liliandaliwa kwa waliojitolea siku hiyo pamoja na wakaazi wote wa lang’ata ambapo zaidi ya wakaazi 400 walijitokeza kupimwa aina mbalimbali za magonjwa.
Darren foundation ilitoa wito kwa wakaazi na wakenya wote kwa ujumla kuwa na uzoefu wa kupanda miti na kutunza mazingira bila kungojea kuitwa.