Home FEATURE STORIES MASAIBU YA JALANG’O KATIKA CHAMA CHA ODM

MASAIBU YA JALANG’O KATIKA CHAMA CHA ODM

0

Mtangazaji wa zamani wa redio na mchekeshaji mashuhuri phelix Odiwuor almaarufu kama Jalang’o amejipata kwenye masaibu tena miezi mitano baadaye.

Munamo mwezi wa nne mbunge huyo alijipata njiapanda baada ya kutangaza msimamo wake wa kushirikiana na serikali kuchapa kazi kwa manufaa ya waliomchagua. Hata hivyo mbunge huyo alizomewa vikali na wanachama wenza wa mrengo wa odm na baadhi ya wafuasi wake kwa tuhuma za kusaliti chama chake cha ODM,kutoka mwezi huo jicho la mrengo wa azimio lilikuwa likimkodolea macho huku uaminifu wake na mrengo wake ukiregarega.

 

Munamo miezi minne baadaye ambapo ni mwezi july Jalang’o alinyenyekea ubavuni mwa mkubwa wake wa chama Raila Odiga walipokutana tena katika  boma la mbunge Caleb Hamisi ambaye alikuwa na tafrija ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya bintiye. Mbunge huyo wa Saboti alikuwa amewaalika wanasiasa kadhaa akiwemo kiongozi wa mrengo wa upinzani wa Azimio la umoja Raila Odinga aliyeitikia wito na kufika katika boma lake na wanachama wengine wa mrengo huo.

 

Hapo ndipo Raila alikutana na Jalang’o ambaye inaarifiwa mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa miezi minne iliyopita alipotoa agizo la mbunge huyo kufurushwa kutoka kwa mkutano wa Azimio uliofanyika kaunti ya Machakos. Wakati wa mkutano huo walinzi wa kiongozi huyo wa upinzani walionekana wakimfurusha Jalang’o kutoka kwa mkutano huo baada ya mbunge huyo na wenzake kukiuka kanuni za chama na kufanya ziara katika ikulu ya Nairobi walikokutana na rais William Ruto licha ya Azimio kipindi hicho kusisitiza kwamba hawakuwa wanamtambua Ruto kama rais wa jamhuri ya kenya.

Mbunge huyo baadae alisisitiza msimamo wake wa kushirikiana na Ruto katika kile alikisema ni kuleta maendeleo kwa wapiga kura wake wa Lang’ata na hivyo kuendelea kupuuza wito wa chama chake kutoshirikiana na serikali. Misururu hiyo ya masaibu imekuwa ikionekana kumkwama Jalang’o  kwani hali si hali siku ya jumatano tarehe 6 mwezi wa September Jalang’o na viongozi wengine wanne walinaswa na mtego wa mrengo wa azimio tena na kufurushwa kutoka kwa chama cha ODM kufuatia mkutano  wa NEC uliofanyika jijini Nairobi.

 

Jalang’o, Mbunge wa Gem Elisha Odhiambo, Mbunge wa Bondo Gideon Ochanda, Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi na seneta wa Kisumu Tom Ojienda wote walitimuliwa kutoka kwa chama hicho kinachoongozwa na aliyekuwa waziri mkuu, Raila Odinga kwa madai ya utovu wa nidhamu na kukaidi msimamo wa chama. Kufuatia hatua hiyo, mtangazaji huyo wa zamani wa redio alizamia kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alishiriki ujumbe wa kujitia moyo.

“Hakuna jaribio ambalo ni nzito sana kuinua!,” Jalang’o aliandika.

 

Mbunge huyo wa muhula wa kwanza aliambatanisha taarifa yake na picha yake ya kumbukumbu ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana ambapo alionekana akiwa amebeba sanduku kubwa la ushahidi mahakamani wakati wa kesi ya Azimio la Umoja dhidi ya ushindi wa Rais aliyemadarakani William Samoei Ruto. Akiongeza kauli yake, Jalang’o pia alishiriki mstari wa Biblia kutoka kwa kitabu cha Wakorintho 10:3 ambao unazungumza kuhusu Mungu kuwasaidia watu Wake kushinda majaribu.

 

“Hakuna jarabio lililokupita ambalo si kawaida ya kwa wanadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hatawaacha mjaribiwe kupita mnavyoweza, bali pamoja na lile jaribio atatengeneza na mlango wa kutokea, ili mweze kulistahimili,” mstari huo wa Biblia unasema.

Katika taarifa yake, chama cha ODM kilisema kuwa waliwatimua viongozi hao watano kwani walipinga maazimio yaliyotolewa na chama hicho.

“Wanachama hao wanakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji wa Ibara ya 11 (1) (e) ya katiba ya chama na kifungu cha 14A cha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2011 kwa kujihusisha na kuunga mkono shughuli za chama pinzani na kupinga maamuzi/maazimio halali yaliyotolewa na chama. vyombo vya chama, wachukuliwe kama wamejiuzulu kutoka chama,” ilisomeka taarifa hiyo. “Chama kinaagizwa kuanza mchakato wa kuwaondoa kwenye daftari la chama.”

Mkutano wa NEC ulioitishwa na Raila mwenyewe ilikuja takriban mwezi mmoja baada ya wanachama hao kufika mbele ya kamati inayoongozwa na Sihanya kujitetea kutokana na shutuma za utovu wa nidhamu