Home HEALTH mfumo wa kidijitali katika sekta ya afya nchini kenya ulivyo muhimu

mfumo wa kidijitali katika sekta ya afya nchini kenya ulivyo muhimu

0

Making Remote Healthcare a Reality in Kenya

Sekta ya afya nchini imekuwa mbioni kukumbatia technolojia ya kisasa sawa na mifumo ya kidijitali kwa lengo la kuimarisha huduma ambazo hutolewa nchini,mojawapo ya mfumo huo ni ule wa kidijitali unaofahamika kama afya KE.Katika hospitali kuu ya kitengela kaunti ya kajiado jukwaa hilo la KE ambalo limekuwa likifanyia majaribio na wizara ya afya katika hospitali hiyo na ile ya chuo kikuu cha Nairobi,imeonekana kupiga jeki na kurahisisha utoaji wa huduma kwenye hospitali hiyo.

Hii ikiwa mojawapo ya ajenda kuu za Rais Wiliam Ruto ambayo ni kuhakikisha kuwa sekta nyingi nchini zinakumbatia mfumo wa kidijitali katika kuendesha shughuli zake,Jukwaa la afya linalo fahamika kama afya KE  ni moja kati ya mabadiliko hayo hasa kwenye sekta ya afya,matumizi ya program hiyo katika hospitali  ya kitengela inaonekana kuongeza juhudi katika utoaji wa hudma.

Michael mona ni afisa msimamizi katika hospitali hiyo ambaye anaelezea kuwa mojawapo ya umuhimu wa mfumo huu katika hospitali hiyo ni iwapo mgonjwa amesajiliwa kumuona daktari inasaidia kuhakikisha kujua mgonjwa ako upande gani wa hospitali na iwapo amehudumiwa au la,pia unasaidia kujua rekodi za mgonjwa iwapo kwanza alikuwa amehudumiwa kajiado na asafiri hadi hospitali nyingine daktari hatakuwa na wakati mgumu wa kujuwa rekodi za mgonjwa kwani zitakuwa zinapatikana katika vituo vyote vya afya nchini.

Kenya | Transform Health

Michael amesema awali hospitali hiyo ilitegemea kuhifadhi maelezo ya wagonjwa  kwenye faili, lakini tangu kuanza kutumika kwa mfumo huo matumizi ya faili na karatasi umeanza kuzikwa katika kaburi la sahau ,huku idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa kwa siku ikiongezeka.Vilevile ameelezea  mfumo huo jinsi unavyotambua aina mbalimbali ya magonjwa ambayo ni sugu katika eneo hilo na hivyo kusaidia kuweka mikakati ya kuyakabili.

Kwa sababu ya usalama wa data, programu hiyo huhifadhiwa kwenye tuvuti kuu ya serikali, hii ikiwa ni kwa mujibu wa sheria ya usalama wadata wa mwaka wa 2019 ambayo inaorodesha data ya wagonjwa kuwa siri ,kando na hayo mfumo huu umebuniwa na kutengenezewa humu nchini na hivyo hauna gharama yoyote kubwa.Tayari kuna baadhi ya kaunti ambazo zinapanga kuanza kutumia mfumo huo kwa lengo la kuboresha  huduma na kupunguza gharama.