Rais William Ruto ameapa kusitisha maandamano kwa kutumia kila njia anayo weza, akidai yanalenga kuharibu mali ya Wakenya wasio na hatia na kumuharibu ajenda yake.Rais alimwambia Raila na waandani wake kukoma kupindua serikali yake kwa kutumia maandamano la sivyo atakabiliana nao ana kwa ana.
Ni kauli ambayo rais amekuwa akirejelea kuwa lengo lake la kusitisha maandamano dhidi ya serikali bado lingalipo, wakati huo rais amesema kuwa serikali itakusanya rasilimali zote kadri inavyoweza kuzima maandamano hayo.
Huku hayo ya kijiri Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki pia amewaonya viongozi wa Azimio na Mkenya yeyote anayepanga kujihusisha katika maandamano “ya uharibifu” kuanzia Jumatano kusitisha nia yake. Msomi huyo wa sheria alisema serikali itakabiliana vilivyo na waandamanaji wote wenye vurugu na haitaruhusu machafuko na uvunjaji wa sheria kutawala.